Hospitali ya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu imeanza kutoa huduma za upasuaji kwa wakinamama wanaopata uchungu pingamizi.

Mganga mkuu wa Wilaya Dk. Anold Musiba amesema huduma hiyo imeanza kutolewa kwa akina mama wajawazito wanaopata changamoto ya kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida lakini pia huduma ya watoto njiti imeaanzishwa hospitalini hapo.

“Tumefanimiwa kuanza kutoa huduma ya upasuaji kwa kina Mama wajawazito wanoshindwa kujifungua kwa njia ya kawaida kutokana na sababu mbali mbali pia tumeanzisha huduma ya watoto njiti pamoja na wale wanaohitaji uangalizi wa karibu sana baada ya kuzaliwa(NICU)”. Amesema Dk. Musiba

Aidha, Dk. Anold Musiba ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna inavyojitoa kuhakikisha huduma bora za afya zinawafikia watanzania wote kokote waliko.

By Jamhuri