Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 16 Januari 2023 amekutana na Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Ikulu Zanzibar.

Uongozi wa Jumuiya hiyo ukiongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Mary Chatanda, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa aliyeambatana na Makamu Mwenyekiti UWT Zanzibar Ndugu Zainab Shomari na viongozi mbalimbali wa kitaifa wa Jumuiya hiyo kwa nia ya kujitambulisha baada ya kuchaguliwa .

Pia wamempongeza Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar na Kutekeleza Ilani ya CCM ya Utekelezaji 2020-2025.

By Jamhuri