Na Mwandishi Wetu, Babati
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Regina Ndege Qwaray amegawa viti 45, kompyuta 36, makabati na meza kwa shule za msingi, sekondari, zahanati na vituo vya Afya, kwenye halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara.
Naibu Waziri Ndege amesema vifaa hivyo amevipata kutoka kwenye taasisi mbalimbali na kuona uhitaji katika shule , zahanati, ituo vya afya vya halmashauri ya wilaya hiyo.
“Nikaona mapungufu katika taasisi zetu za serikali nikaongea na wadau mbalimbali wa maendeleo wametusaidia katika kupunguza mahitaji ya vifaa hivyo kwenye sekta ya elimu na afya,” amesema.
Amewaasa viongozi wa taasisi hizo zilizopatiwa vifaa hivyo kuvitunza ipasavyo wakati wa matumizi yao ili viweze kutumika kwa muda mrefu kwa maendeleo yao na wengine.
Hata hivyo, amewapongeza watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Babati kwa kujituma, kufanya kazi na kutatua changamoto za jamii inavyotakiwa.
Amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kujenga mahusiano mazuri kati yao na watumishi wengine na wananchi kwa ujumla ili kujiletea maendeleo.
“Watumishi mnapaswa kujithamini na kupenda kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha kwamba kila mmoja anatimiza wajibu wake ipasavyo kwenye utumishi wao,” amesema.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, John Noya amemshukuru Naibu Waziri Ndege kwa misaada aliyotoa kwa taasisi hizo za serikali.
‘Tunashukuru sana kwa msaada huu mkubwa, uliotoa katika sekta hizo za elimu na afya kwani changamoto ya upungufu wa vifaa ni kubwa,” amesema Noya.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Anna Mbogo amemshukuru Naibu Waziri Rejina kwa msaada huo na kuomba ushirikiano huo uendelee.
Mkazi wa eneo la Dareda, Victoria Thomas amesema Naibu Waziri Ndege ambaye pia ni mbunge wa viti maalum mkoa wa Manyara mara nyingi amekuwa mtu mwenye moyo wa kujitoa kwa jamii



