Home Kitaifa HUKUMU YA SCOPION YAPIGWA KALENDA HADI JANUARY 22

HUKUMU YA SCOPION YAPIGWA KALENDA HADI JANUARY 22

by Jamhuri

Hukumu ya mwalimu wa sanaa ya kujihami ‘martial arts’  Salum Njwete maarufu kama Scorpion, ya kumjeruhi na kumtoboa macho kinyozi Said Mrisho leo ilishindwa kusomwa katika Makahama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mfawidhi wa wilaya Flora Haule, imeahirishwa hadi January 22 ambapo hakimu huyo atakuwa katika nafasi nzuri ya kuwasilisha hukumu ya kesi hiyo.

Baada ya kuahirisha kesi hiyo Mshitakiwa Scorpion amerejeshwa Rumande hadi January 22 ambapo atasomewa hukumu ya kesi inayomkabili ya kujeruhi na kumtoboa macho Kinyozi Said Mrisho.

You may also like