Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi- Dar es salaam.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillius Wambura amepokea tuzo kutoka kwa chama cha watu wenye wenye ulemavu wa ngozi Tanzania (TAS) ambayo ilitolewa katika maadhimisho ya kumi nane ya kimataifa katika siku ya watu wenye ulemavu wa Ngozi dunuani yaliyofanyika tarehe 13 Juni mwaka huu kitaifa Songea Mkoa wa Ruvuma.

IGP wambura amepokea tuzo hiyo kutoka kwa Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Dk. Lazaro Mambosasa ambapo tuzo hiyo ilipokelewa na Mkuu wa Kituo cha utafiti cha Jeshi la Polisi kilichopo chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam tarehe 13 Juni katika siku ya watu wenye ulemavu wa Ngozi.

IGP Wambura ameongeza kuwa tuzo hiyo imetolewa kutokana na mchango mkubwa wa Jeshi la Polisi katika kuwalinda na kudhibiti vitendo vya ukatili na mauaji ya dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi katika maeneo mbalimbali hapa Nchini.

Kwa upande wake Profesa Semboja Haji ambaye ni mshauri wa Jeshi la Polisi na kituo cha utafiti cha Jeshi hilo amesema Jeshi hilo linakila sababu kwa sasa kujikita katika tafiti ambazo zitaleta matoke Chanya katika utendaji kazi za Jeshi la Polisi huku akiwaomba wakufunzi wa chuo hicho wajikite katika tafiti ili kuendeleza taaluma ya Polisi yenye maboresho katika kutoa huduma bora kwa wananchi Pamoja na mawazo Chanya katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu hapa Nchini.

Nae Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam Kamishna msadizi mwandamizi wa Polisi SACP Dk. Lazaro Mambosasa amesea chuo hicho kimejipanga na kitaendelea kushirikiana na Taasisi za elimu ili kubadilishana uzoefu katika maswala ya tafiti mbalimbali.

Sambamba na hilo Mkuu wa kituo cha utafiti cha Jeshi la kilichopo chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) Kamishna msadizi wa Polisi ACP Ralph Meela amebainisha kuwa kituo hicho kitakuwa na jukumu la kufanya tathimini ya matukio ya kihalifu ambapo amesema kituo hicho kitasadia Jeshi la Polisi pamoja na wananchi kwa ujumla katika kukabiliana na uhalifu hapa Nchini.

By Jamhuri