Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kimeahidi kuongeza ubunifu, kuimarisha ushirikiano na kutumia fursa za rasilimali za ndani katika kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Ahadi hiyo ya JET, imetolewa na Mkurugenzi wake, John Chikomo mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa ufunguzi wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika Septemba 30,2026 mkoani Dar es Salaam.


Chikomo amesema, JET imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inakuwa mstari wa mbele katika kuuhabarisha umma juu ya umuhimu wa miradi mtambuka ya maendeleo ambayo kimsingi inagusa maisha ya wananchi moja kwa moja.

“Kwa miaka mingi sasa JET imekuwa mdau mkubwa wa Habari kwenye maeneo mbalimbali hasa yake yanayogusa mazingira na maisha ya watu moja kwa moja, ahadi yangu kwa serikali ya mkoa wa Dar es Salaam na nchi kwa ujumla, tutaendelea kuongeza ubunifu, kuimarisha ushirikiano na kutumia fursa za rasilimali za ndani katika kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.”

Aidha JET kimealikwa kushiriki na kuunga mkono kampeni mbalimbali za utunzaji na usafishaji wa fukwe, ikiwa ni sehemu ya mikakati endelevu ya kulinda mifumo ya ikolojia ya bahari na ukanda wa pwani nchini.

Kampeni na juhudi za usafi wa mazingira na fukwe katika Wilaya ya Kigamboni zinasimamiwa kwa karibu na uongozi wa wilaya hiyo chini ya Mkuu wa Wilaya, Mhe. Dalmia Mikaya, na Manispaa ya Kigamboni ili kufanya eneo hilo kuwa safi na salama

MIKAYA ATOA WITO

Akifungua mkutano wa jukwaa hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mikaya Tumaini Dalmia, ambae alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, alizitaka NGOs zinazofanya kazi katika Mkoa wa Dar es Salaam kuongeza ubunifu, kuimarisha ushirikiano na kutumia fursa za ndani za rasilimali ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Amesema mashirika yanayofanya kazi katika sekta za afya, elimu, mazingira, uwezeshaji wa kiuchumi na kupambana na ukatili wa kijinsia yanapaswa kutumia fursa zilizopo ndani ya jamii kubuni suluhisho endelevu kwa changamoto zinazowakabili wananchi ikiwa ni pamoja na kuweka bajeti zinazoakisi Dira 2050.

Aidha, Mikaya amezitaka NGOs ambazo bado hazijakamilisha taratibu za usajili na kupata vibali kufanya hivyo kwa wakati na kuzingatia sheria, kufanya kazi kwa kufuata maadili ya Kitanzania, kuwasilisha ripoti za robo mwaka, nusu mwaka na za mwaka, kuwasilisha taarifa za Kifedha, kuwasilisha Mikataba ya Fedha za Miradi, kuwasiliana na Wizara za Kisekta.

Amehimiza pia Mashirika yasiyo ya Kiserikali Tanzania kutokufanya au kujihusisha na shughuli za Kijasusi.

Mikaya amesema NGOs zinapaswa kubuni miradi na fursa za kiuchumi zitakazowasaidia kujitegemea kifedha na kupunguza utegemezi wa wafadhili wa nje.

MASHIRIKA YAPONGEZWA

Mikaya pia, ameyapongeza Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Mkoa wa Dar es Salaam ikiwepo (JET) kwa kuchochea maendeleo ya mkoa na Taifa kwa ujumla.

Katika uzinduzi huo uliobeba kauli mbiu ya “Fikra Mpya kuhusu Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali: Ubunifu, Ubia na Upatikanaji wa Rasilimali Fedha kupitia vyanzo vya Ndani.”

Amesema Serikali inatambua kazi kubwa zinazofanywa na mashirika yanayofanya kazi katika sekta za afya, elimu, mazingira, uwezeshaji wa kiuchumi na kupambana na ukatili wa kijinsia yanapaswa kutumia fursa zilizopo ndani ya jamii kubuni suluhisho endelevu kwa changamoto zinazowakabili wananchi.

Mikaya ameyataka mashirika kutumia ubunifu katika utendaji wa kazi zao ikiwamo kutumia fursa ya mikutano ya Wakuu wa Wilaya kama nyenzo ya kuhamasisha jamii wanazozihudumia ili kufikisha ujumbe wao.

Ameongeza kuwa ni vizuri Mashirika hayo yajitambulishe na kutambulisha shughuli zao kwa Wakuu wa Wilaya wanazofanyia kazi.

NGO ZITAFUTE SULUHISHO

Katika mkutano huo, Mikaya amezitaka NGOs zinazofanya kazi katika Mkoa wa Dar es Salaam kuongeza ubunifu, kuimarisha ushirikiano na kutumia fursa za ndani za rasilimali ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Amesema mashirika yanayofanya kazi katika sekta za afya, elimu, mazingira, uwezeshaji wa kiuchumi na kupambana na ukatili wa kijinsia yanapaswa kutumia fursa zilizopo ndani ya jamii kubuni suluhisho endelevu kwa changamoto zinazowakabili wananchi ikiwa na kuweka kipaumbele bajeti ziwe zinaakisi Dira 2050.

Washiriki pia wamejadili taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mashirika kwa mwaka 2025, ikiwemo mafanikio, changamoto na mipango ya kipindi kijacho.

Aidha, Mikaya amezitaka NGOs ambazo bado hazijakamilisha taratibu za usajili na kupata vibali kufanya hivyo kwa wakati na kuzingatia sheria, kufanya kazi kwa kufuata maadili ya Kitanzania, kuwasilisha ripoti za robo mwaka, nusu mwaka na za mwaka, kuwasilisha taarifa za Kifedha, kuwasilisha Mikataba ya Fedha za Miradi, kuwasiliana na Wizara za Kisekta.

Amehimiza pia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Tanzania kutokufanya au kujihusisha na shughuli za Kijasusi.

Mikaya amesema NGOs zinapaswa kubuni miradi na fursa za kiuchumi zitakazowasaidia kujitegemea kifedha na kupunguza utegemezi wa wafadhili wa nje.

HALI YA USAFI

• Kampeni ya Kila Ijumaa: Viongozi na wananchi wamekuwa wakishiriki kwenye Kampeni ya Usafi ya Kila Ijumaa katika maeneo mbalimbali yakiwemo maeneo ya feri, fukwe, na kata kwa kata.

• Maeneo ya Pwani na Fukwe: Vijana na wakazi wa Kigamboni wamekuwa wakifanya usafi wa mara kwa mara katika fukwe za Bahari ya Hindi zinazozunguka wilaya hiyo (kama vile Kigamboni, Tungi, Vijibweni, na Mjimwema) ili kupunguza taka ngumu na plastiki zinazotapakaa fuvuni.

• Maagizo na Marufuku: Mkuu wa Wilaya amepiga marufuku utupaji holela wa taka na ujenzi usio rasmi kwenye maeneo ya wazi au pembezoni mwa fukwe na maeneo ya biashara.

• Uboreshaji wa Miundombinu ya Majitaka: Jitihada mpya zinaendelea kuwekwa ili kurahisisha usimamizi wa taka na majitaka ndani ya Kigamboni na kupunguza changamoto za kimazingira.

Mikaya amesema JET ina nafasi muhimu katika kuelimisha jamii kuhusu athari za shughuli za binadamu kwa mazingira, hususan uharibifu wa vyanzo vya mito unaoweza kuhatarisha upatikanaji wa maji na kuongeza athari za ukame na uchafuzi.

Mikaya amesema NGOs zinapaswa kuiishi na kuifuatilia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (DIRA 2050) iliyozinduliwa na Mh. Rais Daktari Samia Suluhu Hassan.