Klabu ya JKT Queens imetinga fainali ya Ngao ya Jamii wanawake 2024 baada ya kuikanda Ceasia Queens mabao 7-0.

Mchezo huo wa kwanza wa nusu fainali Ngao ya Jamii wanawake umefanyika wenye uwanja wa KCM, Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo JKT Queens inasubiri mshindi ya nusu fainali ya pili ya dabi ya Kariakoo kati ya Simba Queens na Yanga Princess inayopigwa baadaye kwenye uwanja huo.

FULLTIME:
JKT Queens 7️⃣-0️⃣ Ceasiaa Queens
⚽️Winfrida Gerald
⚽️Anastazia Katunzi
⚽️Stumai Abdallah
⚽️Stumai Abdallah
⚽️Stumai Abdallah
⚽️Janeth Matulanga

Michezo hiyo ni kiashiria cha ufunguzi wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara msimu wa 2024/2025 mwezi huu.

Please follow and like us:
Pin Share