Mbunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Joshua Nassari leo Februari 6, 2018 amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru kusomewa shitaka linalomkabili.

Katika kesi hiyo, Nassari anakabiliwa na tuhuma za kumshambulia na kumsababishia maumivu kwa aliyekuwa Mtendaji wa Kata ya Makiba mwaka 2014, Neema Ngudu. Aidha, Nassari ameachiwa kwa dhamna na kesi hiyo kuahirishwa hadi Machi 6, itakapotajwa tena.

By Jamhuri