Mchuano wa Bayern Munich ya Ujerumani na Arsenal ya Uingereza uliofanyika Jumatano ya Machi 13, mwaka huu, umeacha kumbukumbu ya pekee katika tasnia ya soka duniani.
Siku hiyo, katika tukio ambalo halikutarajiwa na wengi, Arsenal ikiwa ugenini iliichapa Bayern Munich mabao mawili bila majibu katika mashindano ya Kombe la Mabingwa Ulaya barani (UEFA).
Mashabiki wa Arsenal na hata wa Baryern Munich nchini, wamekiri wazi kuwa ufundi uliooneshwa na wachezaji wa timu hiyo ya Uingereza katika mchezo huo ulistahili kuipatia ushindi.
“Ni mechi iliyonivutia zaidi kuitazama miongoni mwa nyingine kadhaa katika mashindano ya UEFA,” amesema mpenzi wa soka wa jijini Dar es Salamaa, aliyejitambulisha kwa jina la John Edward.