Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) imelaani vikali tabia mpya na mbaya inayofanywa na baadhi ya watu wasio waadilifu kutumia mitandao ya kijamii kutukana viongozi wa kiserikali ikiwemo Mhe Raia Dkt Samia Suluhu Hassan.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa JUMIKITA Shabani Matwebe wakati akizungumza na Waandishi wa habari amesema wamekaa kikao na kukubaliana kwa kauli moja kukemea na kulaani vikali sana tabia mpya na mbaya inayotaka kujitokeza nchini matusi mitandaoni dhidi ya viongozi wa serikali.

“Hivi karibuni kumezuka tabia mpya ya watu badala ya Kujadiliana kwa hoja, kutoa mawazo yao au kukosoa Serikali
kwa mujibu wa katiba yetu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 18(1) inayotoa uhuru wa kila Mtanzania kujieleza lakini uhuru unatumika vibaya” amesema Shabani.

Sanjari na hayo Shabani amesema watu hao wamevuka mipaka na wameanza kutukana matusi mazito kwa watanzania wenzao na viongozi wao na wakubwa wao katika umri kinyume kabisaa na Utamaduni wetu, mila zetu na desturi yetu kama Watanzania inayotutaka kuheshimiana sisi kwa sisi wadogo lakini pia kuheshimu watu waliawazidi umri Jambo hili likiachwa linaweza kuhatarisha usalama wa Taifa letu na kuleta maafa makubwa katika Jamii yetu au Nchi yetu.

“JUMIKITA inajua siyo Viongozi wote wataweza kuvumilia kuona wao wanatukanwa au wazazi wao kutukanwa
matusi mazito mbele ya hadahara.
Jambo hili ni hatari na kama litaachwa liendelee kisha likaenea kwa Wananchi kuwa na utamaduni wa kutukanana
wao kwa wao au Kutukana Viongozi wa Nchi kama utamaduni mpya wa Nchi yetu kinaweza kupoteza Amani ya
Nchi yetu” amesema Mwenyekiti

Aidha wito unatolewa kwa Kundi la viongozi wa Dini pia ni Muhimu lisilae kimya wala lisikae pembeni katika kukemea swala hili la matusi mitandaoni kuongea na waumini wao kwa Dini zao na madhehebu yao kama sehemu ya kusimamia maadili ya waumini wao.

By Jamhuri