Na Suzy Butondo JamhuriMedia, Shinyanga

Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini imeteuwa kamati ndogo ndogo ambazo zitasaidia kufanya kazi za maendeleo na kuweza kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii ya Shinyanga mjini.

Katibu wa Umoja wa wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Dorisi Kibabi amezitaja kamati hizo kuwa ni kamati ya uchumi na fedha, kamati ya elimu mafunzo na utamaduni,kamati ya malezi ya watoto, vijana na wazee, kamati nyingine ni kamati ya afya na mazingira.

Kibabi amewataja wajumbe wa kamati ya uchumi na fedha kuwa ni Salumu Jambo,Gift Njau, Della compan limited,Alice Salvatory, Gilbebert oscar Mlekwa,Lucy Mwita,Joseph Temela,Doris Mosha,John Ntalimbo, Mserikali Kahitira Gamba na Mary Izengo ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati hiyo.

Wajumbe wa kamati ya elimu, mafunzo na utamaduni ni Bahati Burongo Dede,Adon Kweka,Mwanaharusi Kulwa, Jonas Jonathan,Varerian Baleke,Sagile wambula Marwa,Annasscholasticka Ndagiwe,Miraji Zahoro Chomoka.

Wajumbe wa kamati ya malezi ya watoto ni Christopher Ringo, Constantine Nkuba,Zamda Shaban, Joseph Mshandete,Zipporah Pabgani, Farisha Fundikila, Juma Machalilu,Anna Shula Selemani Furana na Daniel Kapaya.

Wajumbe wa kamati ya Afya na mazingira Emmanuel Mwandu,Valentine Mussa Mahuna,Maxwell Faraja, Daniel Isack Mzera, Vivian Zabron Mwendo,Consolata Faustine Nangale,Herena Swai, Jimotoli Jilala,Zephania Magara Gumje Debora Mpanduji, Pili Charles.

Wajumbe wote walioteuliwa wameushukuru uongozi kwa kuwateuwa na kuahidi kwamba watashirikiana kwa pamoja na Jumuiya hiyo ili kuhakikisha wanaibua mambo mbalimbali na kutatua changamoto zote za kijamii zinazowezekana kutatuliwa.

Mjumbe wa kamati ya malezi watoto, na vijana na wazee Kostantine Mollo Nkuba amesema watahakikisha uchumi unakuwa na wataendelea kujengeana uwezo ili waweze kukuza fursa kwani zipo zaidi ya120 na watafanya ubunifu wa kuibua changamoto mbalimbali ili ziweze kufanyiwa kazi.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Fue Mrindoko amefurahishwa na wajumbe wa kamati hizo kwa kuwa tayari na kukubaliana kufanya mambo makubwa ya kuijenga Jumuiya hiyo na kutatua kero mbalimbali zilipo katika jamii na kuielimisha jamii kuondokana na mira potofu.

“Niwaombe mkatekeleze majukumu yenu yote mliyojipangia ili kuhakiksha tunaweka alama katika kufanya maendeleo na kushughulikia kero mbalimbali katika jamii yetu,”amesema Mrindoko.

Kwa upande wake katibu Kibabi amewaomba wakatoe elimu kwenye jamii ili baadhi ya wanaume wanaojigeuza kuwa wanawake waache mara moja tabia hizo kwani tabia hizo ni za udhalilishaji na ni aibu kubwa katika jamii ya kiafrica na kufanya hivyo ni kupoteza nguvu kazi ya Taifa.

“Kuna baadhi ya wanaume wanabadili asili yao na kuanza ushoga, hili ni jambo baya la udhalilishaji na ni la aibu kabisa katika Taifa letu, kwani wanaume wakijigeuza wanawake, idadi ya wanaume inapungua, hivyo nendeni mkafikishe elimu mashuleni magulioni na sehemu mbalimbali ili wanaume wasiendelee kufanya tabia hii,”amesema Kibabi.