Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia, Dar es Salaa

Serikali ya Tanzania kupitia Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania( JWTZ linatarajia kufanya maadhimisho ya miaka 60 tangu kuasisiwa kwake Septemba 1, 1964 na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es salaam Julai 3 ,2024, Kaimu Mkurugenzi wa habari na uhusiano wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania( JWTZ) ambaye pia ni Msemaji wa Jeshi hilo Luteni Kanali Gaudentius Ilonda amesema maadhimisho hayo yanayotarajiwa kuanza kamandi zote za kijeshi zitahusishwa ikiwemo ya jeshi Anga, nchi kavu, Jeshi la akiba, wanamaji (Baharini) na vikosi maalumu vya ulinzi na itafanyika katika mikoa Dar es Salaam,Tanga,Morogoro,Pwani na katika maeneo hayo watashuhudia baadhi ya kazi za kijeshi hivyo wasiwe na wasiwasi waendelee na shughuli zao za kila siku za kiuchumi kwani hakuna atakayedhuriwa.

Sambamba na hayo Luteni Kanali Ilonda amesema shughuli zote na matukio yote ya maadhimisho yatafunguliwa Julai 25,2024 na kuhitimishwa Agosti 23,2024 hivyo kutakuwa na sherehe kadha wa kadha ikiwemo Mashindano Utamaduni ya Mkuu wa majeshi kwa mara kwanza pia yakiambatana na mchezo wa CDF Cup

Luteni Kanali Ilonda amesema maadhimisho hayo yataenda sambamba na shughuli mbalimbali za kijamii kama vile utoaji wa matibabu kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya kutoa shukrani kwa wananchi kwa kuendelea kudumisha amani na mshikamano na Jeshi hilo tangu kuanzishwa kwake.

“Utoaji wa huduma bure kwa wananchi Hospitali zote za Kanda za Kijeshi ikiwemo Arusha,Mwanza,Mbeya,Tabora,Zanzibar,ttutatoa matibabu bure kwa wananchi ikiwemo magonjwa ya kuambukiza kama vile UKIMWI, na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile Shinikizo la Juu la Damu,Saratani ya Matiti,Tezi dume,Sukari, Maabara ya damu salama pamoja na magonjwa ya dharura,hivyo nawaomba wananchi kujitokeza kupata huduma hizi na ushauri nasaha ” amesema Luteni Kanali Ilonda.

Luteni Kanali Ilonda amesema kuwa katika maadhimisho hayo kutakua na mazoezi mbalimbali ya kivita yatakayofanyika katika Mikoa ya Dar es salaam,Pwani,Tanga na Morogoro hivyo amewaomba wananchi wasiwe na hofu pindi watakapoona zana za kivita ikiwemo magari vifaru na ndege vita zikipita katika makazi yao.

” Naomba niwatoe hofu wananchi wanapoona zana za kivita zinapita kwenye maeneo ya makazi yao msiwe na hofu muendelee na shughuli zenu za kiuchumi kama kawaida kwani zana hizo zinatumika tu katika zoezi la maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi lao,ambapo mwaka huu tunataka maadhimisho haya yawe ya aina yake tofauti na maiaka mingine.

Katika hatua nyingine Jeshi la Ulinzi la wananchi Tanzania watashirikiana na Jeshi la Ulinzi Ukombozi wa watu wa kufanya zoezi la Mataifa yote hayo mawili hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ambapo wataanza Julai 29,2024 na kuhitimishwa Agosti 11 mwaka huu katika Mkoa wa Dar es salaam na Pwani na kamandi mbalimbali zitakazohusika ni pamoja ikiwemo Jeshi la Anga , Wanamaji, nchi kavu huku zana zitakazotumika ni Meli vita na Ndege.

” Zoezi hili la Serikali kupitia JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China kwa kuwakumbuka waasisi wa majeshi haya akiweo Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa China wa awamu hiyo,lakini pia ni kumbukumbu ya miaka sitini ya JWTZ tangu kuanzishwa kwake,na pia ni kumbukumbu ya miaka sitini ya udugu na uhusiano wa mataifa haya mawili” amebainisha Luteni Kanali Ilonda.

Nakuongeza kuwa” Zoezi hili litafanyika Baharini na Nchi kavu hivyo litafanyika kwa uwazi ili wananchi wapate fursa yakujionea kupitia vyombo vya habari kwa wale ambao hawapo maeneo ya Baharini,lakini wale ambao wapo karibu na maeneo ya Baharini itakua fursa kwao kuona mbashara na itakua sehemu ya utalii kwao.

Sanjari na hayo amesema kutakuwa na utoaji huduma za matibabu bure ambapo Meli kutoke nchini China ya Matibabu itawasili Julai 16,2024 hivyo wananchi wote wanakaribishwa kufika kutibiwa na kutalii katika meli hiyo kwani ni fursa adhimu Jeshi limeandaa na Maandalizi yote yameshakamilika

Aidha Maadhimisho hayo yataongozwa na kauli mbiu isemayo” Miaka 60 JWTZ umoja,nidhamu,utii,uhodari, ni msingi wa Jeshi letu katika katika kuadhimisha ulinzi, amani na utulivu na kilele chake ambayo ndiyo siku yenyewe ya maadhimisho septema 1, kutafanyika gwaride maalumu pamoja na kuonyesha silaha zote za kivita kuanzia JWTZ ilivyoanza na ilipo sasa.katika kuimarisha ulinzi