*Sasa hakuna kutorosha jiwe nje ya uzio
*Wazalendo furaha, wakwepa kodi kilio

SIMANJIRO

NA MWANDISHI WETU

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) limepokewa kwa shangwe kwenye
dhima yake mpya ya kulinda migodi ya
tanzanite, Mirerani mkoani Manyara.
Uwepo wa askari wa JWTZ wenye silaha na
magari ya deraya katika eneo hilo, ni
utekelezaji wa maagizo ya Amiri Jeshi
Mkuu, Rais John Magufuli, Aprili 6, mwaka
huu alipokuwa akizindua ukuta uliojengwa
kuzunguka eneo hilo. Ukuta huo wenye
kimo cha mita tatu na urefu wa kilometa

24.5; umegharimu Sh bilioni 6.
Katibu wa Chama cha Wachimba Madini
Mkoa wa Manyara (MAREMA), Tawi la
Mirerani, Abubakari Madiwa, amezungumza
na JAMHURI mwishoni mwa wiki na
kusema wamefurahi mno kuona eneo hilo
linalindwa na JWTZ.
“Kuna magari ya deraya na askari wenye
silaha za kawaida, kwa kweli wachimbaji
wamefurahi ingawa yapo malalamiko
madogo hasa kwenye upekuzi kwa kina
mama.
“Wamefurahi kwa sababu wanasema ni
tofauti na polisi. Si wasumbufu sana,
wanataka ukweli tu. Ukifika unaambiwa
nenda pale, lipia, ondoka, hakuna
longolongo,

” amesema Madiwa.

Ameulizwa kwanini polisi wanalalamikiwa
na wachimbaji wadogo na kujibu:
“Wanasema [wachimbaji] wao huwa
wanataka hela, mara hela ya kula, mara
hela ya maji, lakini Jeshi (JWTZ) hawana
hayo.”
Hata hivyo, Madiwa amesema kumekuwapo
malalamiko ya hapa na pale hasa kutoka
kwa kina mama.

“Wanaona kupekuliwa hadi kwenye ‘duka’
[sehemu za siri] si jambo zuri.
Wanapendekeza ingekuwa vizuri
wakatumia scanner ambazo zina uwezo wa
ku-detect chuma au madini,

” amesema.

Ukiacha dosari hiyo aliyosema
inarekebishika, katibu huyo amesisitiza:
“Jeshi tumelipokea kwa mikono miwili.
Tuliahidi na tunaendelea kuahidi kuwa
tutafanya kazi nalo kwa karibu. Sisi
tutakuwa walinzi namba mbili ili kuhakikisha
kuwa hakuna madini yanayotoroshwa. Awali
tulitaka tulinde sisi lakini tukawa tunatupiana
mpira hasa kwenye gharama za kuwalipa
walinzi, lakini Mheshimiwa Rais (Magufuli)
aliposema JWTZ watalinda, kwa kweli
tulifurahi na sasa tunaiona kazi yao,

amesema.
Wiki iliyopita, Msemaji wa JWTZ, Kanali
Ramadhan Dogoli, alisema idadi ya askari
imeongezwa kwenye migodi ya Mirerani ili
kuimarisha ulinzi. Akakanusha kuwapo kwa
vifaru.
“Hatuwezi kuimarisha ulinzi hata mara moja
kwa kutumia vifaru, vifaru na ukuta
haviendani kabisa, vifaru viko mbali

[Arusha],

” amesema.

Baadhi ya wachimbaji wadogo
waliozungumza na JAMHURI
wamepongeza uamuzi wa kupelekwa askari
wa JWTZ kulinda