Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga akizungumza na Wajumbe wa Kampuni ya kutengeneza Nguzo za Zege Tanzania (TCPM), na Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme (ETDCO), (hawapo pichani) wakati wa kikao kilichofanyika Tarehe 04 Januari 2024, katika Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati Jijini Dar Es salaam.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme (ETDCO),  Mohamed Abdullah akitoa taarifa kuhusu utendaji wa kampuni hiyo kwa Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga wakati wa kikao kilichofanyika Tarehe 04 Januari 2024 katika Ofisi za Wizara ya Nishati Jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya kutengeneza Nguzo za Zege Tanzania (TCPM),  Mha. Yusuph Kitivo akitoa taarifa kuhusu utendaji wa kampuni hiyo kwa Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga wakati wa kikao kilichofanyika Tarehe 04 Januari 2024 katika Ofisi za Wizara ya Nishati Jijini Dar es Salaam.

……………………………

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia,

Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga ameziagiza Kampuni za kutengeneza Nguzo za Zege Tanzania (TCPM) na Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme (ETDCO) kutekeleza kile walichokikusudia kwa maslahi mapana ya nchini yetu.

ETDCO na TCPM ni Kampuni Tanzu za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)

Mhe. Kapinga ametoa wito huo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na kampuni hizo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Nishati, Jijini Dar Es Salaam, Tarehe 4 Januari, 2024.

Ameielekeza TCPM ambayo kuwa makini na kufanya uchaguzi sahihi wa kampuni zenye uwezo watakazoingia nazo ubia au mikataba katika kufanya nao kazi husika.

Pia Ameielekeza ETDCO kukamilisha kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa miradi yote ya kipaumbele ambayo wanaitekeleza.

“Mnapoingia Ubia na kampuni fulani muwe makini na kampuni zenye sifa, msifanye uchaguzi wa kubebana wala kupendeleana au kupewa maagizo. Simamieni misingi yenu ya kazi, ili kupata wabia wenye uwezo wa kufanya kazi, kwa hapa tulipo hatuhitaji ubia wa wabia wasio na uwezo wa kifedha na kazi”, Alisisitiza Mhe. Kapinga.

Mtambue kuwa fedha mtakazopatiwa kwa ajili ya kutekeleza miradi yenu ni fedha za Serikali hivyo zitumike kwa tija na kuleta matokeo chanya. Kile kizuri mliochokiandika katika makaratasi kiendane na utekelezaji