Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Songea

WANANCHI wa Kata ya Matimila wilayani Songea mkoani Ruvuma wameipongeza Serikali kwa kuwaboreshea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa zahanati na kituo cha afya cha kata hiyo ambacho kimewarahisishia kupata matibabu karibu tofauti na  ilivyokuwa awali walikuwa wakienda Songea mjini kwenye hospitali ya Mkoa (Homso) yenye umbali wa zaidi ya kilomita 30.

Pongezi hizo zimetolewa jana na Mariam Komba mkazi wa Kijiji cha Matimira B wakati wa ziara ya mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama ambaye pia ni Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na Uratibu ambapo alitembelea zahanati ya kijiji hicho ambayo ujenzi wake upo kwenye hatua za mwisho ambapo hadi kukamilika ujenzi huo utagharimu kiasi cha shilingi zaidi ya Milioni 50.

Jengo la zahanati ya kijiji cha Matimila B iliyopo katika halmashauri ya Songea

Komba amesema katika kuchochea maendeleo ya ujenzi wa kijiji hicho tayari wananchi wa kikjiji cha Matimira B wameoneshwa kufurahishwa na miradi huo ambao ukikamilika utaweza kuwaondolea adha waliokuwa wanaipata kwenda umbali wa kilomita zaidi ya 30 kupata matibabu pale wanapokuwa na matatizo ya kuumwa. 

Sophia Haule mkazi wa Kijiji hicho amesema mradi huo endapo utakamilika utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa akina mama wajawazito ambao walikuwa wanalazimika kwenda kusuburia muda wa kujifungulia wakiwa jirani na hospitali ya mkoa jambo ambalo limekuwa ni kero kwao.

Akitoa taarifa ya ujenzi wazahanati ya Kijiji hicho kwa Mbunge na Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri mkuu sera,Bunge na uratibu Jenista  Mhagama  Ofisa Mtendaji wa Kata ya Matimila Omary Kamale kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya zahanati hiyo amesema kuwa wananchi wa kijiji hicho wameshiriki kwa kiasi kikubwa kulisafisha eneo hilo kisha walichimba msingi wa jengo hilo na kuanza kufyatua tofari kisha walianza kujenga jengo hilo.

Kamale amefafanua kuwa walipokea fedha kiasi cha sh. Milioni 1.5 toka halmashauri ya Wilaya ya Songea ambazo zilisaidia kubebea tofari kuleta kwenye eneo la ujenzi  pia kijiji kilipokea fedha kutoka serikali kuu kiasi cha sh.milioni 50 ambazo zimesaidia kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa zahanati hiyo mpaka kufikia hatua lililopo na kwamba pia halmashauri ilileta fedha sh.milioni 15 ambayo nifedha ilyotokana na mapato ya ndani kwa lengo la kukamilisha ujenzi ambao unaendelea katika hatua za mwisho na kuanza sasa muda wowote itaanza kufanya kazi.

Ofisa mtendaji wa Kijiji hicho Kamale alisema kuwa wananchi wa kijiji hicho kupitia mkutano wao wa hadhara uliofanyika Agost 19 mwaka huu pia walikubaliana kujenga nyumba ya watumishi wa zahanati hiyo hivyo kuanzia Oktoba mwaka huu ujenzi wa nyumba hiyo utaanza rami kujenga mbili kwa moja(two in one)ili kuleta ufanisi kwa watumishi katika utendaji kazi ambapo mpaka sasa kuna sh.milioni 5.5 ambazo zimetengwa na zipo zipo benki.

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri mkuu sera,uratibu na Bunge ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Peramiho Jenista Mhagama akiwahutubia wana nchi wa kijiji cha Matimila B mara baada ya kuweka jiwe.jiwe la msingi.

Kwa upende wake mbunge wa Jimbo la Peramiho na Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri mkuu sera,Bunge na uratibu Bi. Jenista Mhagama ameahidi kutoa mabati 200 kwaajiri ya nyumba mganga pamoja na watumishi wa zahanati hiyo pia ameahidi kutoa vitanda kwaajiri ya akina mama wajawazito na amewaagiza shirika la umeme (Tanesco)kupeleka umeme haraka iwezekanavyo ili huduma kutolewa masaa 24 na si vinginevyo.

Ameuagiza uongozi wa halmashauri hiyo kuona umuhimu wa kuchukuwa hatua za haraka kuhakikisha kuwa vifaa tiba kwaajiri ya zahanati hiyo vinapatikana ili baada ya kufunguliwa wananchi wasipate adha hiyo tena ya kufuata huduma maeneo mengine. 

By Jamhuri