Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia, Dar es Salaam

Vijana wameshauriwa kuanzia mwaka huu 2024 waache kulalamika kuwa hawapewi nafasi za uongozi hivyo wajitokeze kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali ili wapate kushika hatamu kuongoza nchi yao ikiwemo ubunge, udiwani, unyekiti wa Serikali za Mtaa .

Ushauri huo umetolewa Julai 6,2014 jijini Dar es Salaam na Katibu NEC Idara ya Organization, Issa Gavu mara baada ya Uzinduzi wa kampeni ya “Tunazima zote tunawasha kijani’ iliyoandaliwa na Umoja wa Vijana UVCCM lengo ni kuwandaa vijana na Uchaguzi Mkuu ambapo amesema vijana hawana budi kuhamasika kilijenga taifa likiwa na viongozi imara wenye nguvu na mawazo chanya wasioyumbishwa na chochote.

“Ukiwa wewe kijana usikae ukazembea fursa hii adhimu ya kuanzia mwaka huu 2024 na kuchagua kugombea kwani nafasi hizi zimeletwa kwa watu wote wenye vigezo sisi tunapenda kuona kuona hawabaki nyuma kwani hatuwezi kupata vijana wazuri nje ya chama cha CCM msizembee” amesema.

Gavu amesem CCM inawapa fursa vijana wote kugombe nafasi mbalimbli za uongozi kwani Tanzania ya leo na kesho inaundwa na hilo kundi endapo wataitumia nafasi hiyo vizuri na wakipat nafasi hawana budi kuendeleza amani umoja na Mshikamano ulipo.

“Serikali ilipo madarakani chini ya Usimamizi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassani imekuwa ikiwatengeneza vijana kuanzia kwenye elimu kwani inawapatia mikopo ya elimu ya juu wasome pia imetenga fedha kila halmashauri fungu ili wajikwamue kiuchumi sasa ukisema wewe ni masikini umejitakia hata kama huna ujuzi wowote” amesema Gavu.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi UVCCM Taifa Mohamed Kawaida amewataka Vijana kuhakikisha Mikoa yote inazimwa na kuwasha Rangi ya Kijani ili kuunga mkono juhudi mbalimbali anazozifanya Rais Samia katika kulijenga Taifa.

Nae Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Jokate Mwegelo amesema Watahakikisha Uchaguzi Mdogo na Mkubwa unaotarajiwa kufanyika Octobar 2025 unaleta mafanikio na Chama kinashinda Kwa kishindo