Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania, Prof. Kenneth Bengesi, amesema wanaendeleza mchakato wa majadiliano na wadau wa sekta hiyo nchini lengo ni kuhakikisha maslahi ya umma na wadau yanalindwa.

Amefafanua hayo Mwishoji wa wiki iliyoipita Julai 5, 2024 mbele ya Wahariri na Waandishi wa vyombo mbalimbali nchini na kuweka wazi anaamni majadiliano hayo yataweza kutatua changamoto zilizokitokeza na kusababjsha uhaba wa Sukari siku chache zilizopita na kufanya kuwepo kwa maneno mengi yanayoweza kuleta taharuki kama hakutakuwa na ufafanuzi kuhusu hali halisi ya kinachoendelea.

“Msimamo wetu na Serikali ni kuhakikisha wananchi, wakulima, wadau tofauti pamoja na wawekezaji wanalindwa na kuweka mazingira katika sekta hii yanayoendana na kukenga mahusiano mazuri kwa maslahi ya watanzania wote na kufanya maboresho kila inapohitajika kufanya hivyo,” amesema.

Ameongeza kuwa sekta hiyo itafanya vema na kupata mafanikio zaidi kupitia majadiliano mbalimbali na wadau kwa maana jambo hilo ni nyeti na muhimu hivyo wanalichukulia kwa umakini kwa umakini mkubwa.

Siku chache zilizopita kumekuwa na mjadala mkubwa ndani ya Bunge na kusababisha kuleta hali ya sintofahamu nchini kuhusu mikataba kadhaa iliyodaiwa kusababisha uhaba wa sukari nchini, ingawa ufafanuzi ambao umetolewa umeweka hali shwari.

Amefafanua kuwa wakati walipaoamua kulegeza mchakato wa uingizwaji wa sukari ilisababisha kuwepo kwa kiasi kikubwa kinachoingizwa nchini na kuyumbisha soko la ndani, hali iliyofanya Serikali kubadilisha Sheria na kubadili mfumo wa uingizaji wa bidhaa hiyo nchini jambo ambalo limesaidia kulinda soko la ndani.

Mkurugezi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania, Prof. Kenneth Bengesi ameeleza kuwa Sheria ya Usalama wa Chakula ilitumika kuingiza Sukari ya Dharura baada ya makampuni (Wazalishaji wa Sukari) kupewa vibali vya kuingiza tani (50,000) na kuishia kuingiza tani elfu sita (6,000) pekee tofauti na vibali vilivyowaelekeza jambo lililopelekea kutokea upungufu wa sukari na bei kuwa juu”

Prof Bengesi Vibali vya kuingiza Sukari nchini vilitolewa mapema kama kawaida lakini baadhi ya Wazalishaji wa Sukari (kampuni nne) ukiondoa ‘Kilombero Sugar’ walioingiza kiasi kidogo’, wengine hawakuingiza Sukari hata tani moja nchini, hali iliyopelekea upungufu na matokeo yake bei ya Sukari ikawa juu.

Baadhi ya watu wanaoelezea suala la sukari hawana taarifa za kutosha, hivyo ni jukumu letu Bodi kutoka hadharani pamoja na mambo mengine, kutoa picha kamili ya namna gani Watanzania wanaenda kupata ahueni kubwa baada ya serikali kufanya mabadiliko katika sheria ya sukari nchini,”Alisema Profesa Bengesi.

Baadhi ya hoja zilizofafanuliwa na Bodi ya Sukari Tanzania ilikumbwa na uhaba wa sukari, malalamiko ya utoaji wa vibali na mbinu zinazoenda kutumika kwa lengo la kuhakikisha bidhaa hiyo kuwa adimu nchini inaenda kuwa historia.

“Mnajuwa dharura tuliyokuwa nayo, tulikuwa kwenye mazingira ya dharura kubwa na ilikuwa ni lazima tuchukue hatua ya dharura kukabiliana na tatizo lililokuwa mbele yetu, unapokuwa katika hali hii hautumii njia za kawaida, yaani nyumba inawaka moto upo ndani afu unatafuta mlango,? unachotafuta namna ya kutoka, kwahiyo sisi tuliangalia mbadala bila kuvunja taratibu” Prof. Kenneth Bengesi, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari