Katibu Mkuu wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Balozi Anda Filip, amefika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kwa ajili ya kukagua maendeleo ya maandalizi ya Mkutano wa 153 wa IPU unaotarajiwa kufanyika jijini Arusha kuanzia Oktoba 5 hadi 9, 2026.
Katika ukaguzi huo, Balozi Filip ameambatana na Balozi wa Tanzania anayeshughulikia Dawati la IPU Geneva, Mhe. Hoyce Temu.
Akizungumza baada ya ukaguzi, Balozi Filip ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Bunge la Tanzania kwa maandalizi yanayoendelea AICC kuelekea Mkutano huo.
Aidha, amewakaribisha wageni wote wanaotarajia kufika jijini Arusha kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 153 wa IPU.
Mkutano huo utajadili kaulimbiu isemayo, “Enhancing good governance and empowering communities through inclusivity, trust and opportunities for all”, na unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya wajumbe 2,000 kutoka katika Mabunge 183 wanachama wa IPU.











