📌 Inajishughulisha na kutoa ushauri Sekta ya Nishati

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amekutana na Wataalam kutoka Taasisi ya Energy CARDS ambao walifika ofisini kwake kwa ajili ya kutambulisha shughuli wanazozifanya.

Katika kikao kilichofanyika tarehe 7 Machi, 2024 jijini Dar es Salaam, Wataalam hao walieleza kuwa Taasisi hiyo inajishughulisha na masuala ya kutoa ushauri wa kitaalam (consultancy) hususani kwenye masuala ya Nishati katika gesi, petroli na nishati jadidifu.

Katibu Mkuu aliwapongeza Wataalam hao na kuwahakikishia kuwa Wizara iko tayari kuwatumia wataalam wa ndani kwa ajili ya miradi mbalimbali.

Baadhi ya Wataalam kutoka Taasisi hiyo ni Gabriel Bujulu, Edward Ishengoma, Mary Pancras, Adam Zuberi, Helen Lyimo, Mha. Kato Kabaka na Jacob Mayalla.