Askari GGM wanatumaliza

Viongozi wa Wilaya ya Geita wajue kuwa askari maarufu kama ambush na wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) wanatutesa sana, baadhi yetu wanafanywa vilema na wengine wanauawa. Wapo watu wengi wamekufa kutokana na kupigwa risasi. JAMHURI tusaidieni kupigia kelele tatizo hili, tunakwisha!

Paulo, Geita

0758 479 354

Heri ukimwi kuliko ufisadi

Afadhali ukimwi kuliko ufisadi. Watanzania hatupendi kuona uchumi wa nchi yetu unawekwa mifukoni mwa wajanja wachache. Mfano mgogoro unaofukuta katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba chimbuko lake ni ni ujanja na ubadhirifu wa mali za umma. Watanzania tushirikiane kupinga ufisadi.

Samwel, Mto wa Mbu – Arusha

0787 683 360

 

Mwakyembe waungwe mkono

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe amekamata dawa za kulevya, sijui kama atapata ushirikiano kutoka kwa wenzake wizarani, Jeshi la Polisi na mahakama. Tusubiri kichekesho kama hatutaambiwa kwamba dawa hizo zilikuwa kemikali ya kutengeneza vitu fulani fulani, tutaduwaa!

Msomaji wa JAMHURI

0757 289 362

 

Magufuli anafaa kuwa rais

Mh! Matukio ni mengi, wa kuyasemea hatumwoni ingawa waandishi wa habari mnafanya kila muwezalo lakini mnaambulia kudhuriwa! Mungu awe mtetezi wenu daima, wananchi tuko nyuma yenu. Nionavyo mimi Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli anafaa kuwa rais wa Tanzania kuanzia mwaka 2015.

Mfuasi wa Chadema

0786 722 031

 

Tusipoziba ufa tutajenga ukuta

Wananchi wa kawaida tunanyanyaswa ndani ya nchi yetu inayotangazwa kuwa ni kisiwa cha amani duniani. Matukio ya watu wasio na hatia kutekwa, kuteswa, kumwagiwa tindikali na kuuawa kikatili. Tusipoziba ufa tutajenga ukuta. Nchi yetu imekuwa na vitendo visivyopendeza hata mbele za Mungu.

Mdau wa JAMHURI

0769 316 154

 

Profesa Lipumba hamjui Ponda

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ni kama hajijui aliko kuhusu sakata la Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda. Asiingize udini katika siasa, masuala ya udini ayaweke kando na siasa vinginevyo ataonekana hafai katika siasa.

Kessy wa Kibamba, Dar es Salaam

0776 624 331

 

Hata choo mnasubiri kujengewe?

Ndugu mhariri, kwanza hongera kwa kazi nzuri ya kutupasha habari. Hapa kwetu kijiji cha Old Shinyanga ofisi za kata za Old Shinyanga na Mahakama ya Mwanzo hazina choo kwa ajili ya huduma za haja kubwa na ndogo. Hali hii inawalazimu wateja wao kwenda kujisaidia jeshini. Hata choo mpaka wajengewe?

Dotto Makaya, Old Shy

0783 698 949

 

Kimondo cha Ndolezi chatelekezwa

Ninashangaa kuona watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania walivyotelekeza maeneo mengi ya kihistoria kikiwamo kile kimondo cha kule Ndolezi-Mbozi, Mbeya pamoja na lile daraja la Mungu kule Tukuyu. Wizara isiyasahau maeneo haya kwani yanaweza kuliongizea taifa kipato.

Emmnuel Louis, Mbozi

1714 477 085

1041 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!