Na Jumanne Magazi, JamhuriMedia, Dar ea Salaam

Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amesema Tanzania iko tayari kuhakikisha inashirikiana na Jumuiya ya Kimataifa ili kudhibiti vyanzo vyote vinavyosababisha majanga na usalama kwenye vivuko vyote Nchini pamoja na kuweka mazingira salama kwenye Vivuko vyote hapa nchini.

Ameyasema hayo leo April 17,2024, wakati wa kufunga semina ya siku mbili ya kikanda inayojumuisha wadau wa usalama wa Vivuko baharini Barani Afrika chini ya Shirika la Kimataifa la Vivuko Duniani (IOM Ferry).

Kihenzile amesema serikali kupitia Ripoti iliyotolewa miaka 2 iliyopita kataka Ziwa VIctoria pekee takribani watu 5000 hufa maji kila mwaka.

Ambapo leo jumla watu wa ndani na nje ya Afrika kutoka nchi 17 na wengine 6 kutaka Uaya wameshiriki semina hiyo, huku lengo kuu la mkutano huo ikiwa kujadili na kujengeana uwezo wa kuhimarisha usalama katika maji yetu ikiwemo bahari, maziwa, na mito ili kujengea uwezo wa kudhibiti ajali na ulinzi na usalama wa binadamu wanaotumia Vivuko hapa nchini.

Aidha Kihenzile ameishukuru Taasisi hiyo ya IMO, pamoja na TASAC, kwa pamoja ambao kimsingi ndio wamekasimiwa kulinda na kuthibiti usalama wa vyombo vya majini pamoja na Vivuko kwenye maziwa bahari na maziwa.

Vilevile Kihenzile amesema kwa sasa Serikali, imetenga kiasi cha zaidi ya Trilioni 1 kwa ajili ya Ununuzi wa meli, huku zaidi ya bilioni 650 kwa ajili kujenga kiwanda cha meli kule mkoani kigoma, na kujenga Meli ya Mizigo ya Tani 3500,katika Ziwa Tanganyika na Ziwa VIctoria “Tunajenga Meli nyingine ya MV Mwanza hapa kazi”

Kando ya hayo Kihenzile amesema kuwa Serikali “Tunakarabati Meli za kutosha katika Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa pamoja na Ziwa VIctoria ili ziweze kutoa huduma Bora na Salama kwa Watanzania.

“Tunaendelea na utafiti katika Bahari ya Hindi, ambako hukui tunatakaweka Meli za kutosha” ambapo kwa Uwekezaji huo Amesema lazima “Tunapaswa kujifunza kulinda watu wetu wakiwemo watumiaji wa vyombo hivyo pamoja na watu wengine waliopo kwenye maji hayo.

Mwisho Naibu Waziri Kihenzile ametoa Rai kwa watumiaji wa Bahari, Maziwa na Mito kufuata Sheria za ndani na zile za Kimataifa ili kuhimarisha usalama wao, Pia ameiomba TASAC kuendelea kusimamia na kulinda usalama wa watumiaji wa maji ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza, Amesema Kihenzile.

Naye Mhandisi Mkuu Kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania,Bw Michael Myaka amesema wao kwenye mkutano huo ni wadau wa kubwa wa Vivuko kwani wanashirikiana na TASAC ambao wao kazi yao ni kudhibiti na kuratibu shughuli zote za vivuko na meli hapa nchini,

By Jamhuri