Chelsea vs Manchester City nani mbabe?

Mashabiki wa kandanda kote dunia wana shauku ya kujua nini ataibuka mshindi kati ya Chelsea (The Blues) ya Stanford Bridge na Matajiri wa London Manchester City, wakati mafahali hao wa England watakapopepetana katika mchuano unaotarajiwa kuwa mkali wa kuwania Kombe la FA.

Chelsea iliyoshiriki fainali za Kombe hilo mara saba na kufanikiwa kulitwaa mara sita, inatarajiwa kupambana na Man City, Mei 11 mwaka huu. Awali Chelsea iliishinda City katika mchezo uliopigwa April 14 katika Uwanja wa Wembley.

 

The Blues katika ushindi wake wa kwanza mwaka 2007, iliishinda timu ngumu ya Manchester United kwa bao 1 bila majibu, na Mwaka 2009 katika mchezo wa nusu fainali kuizamisha Arsenal kwa mabao 2-1. Mwaka 2009 katika fainali, iliibugiza Everton 2-1. Mwaka huo huo iliipiga kumbo Aston Villa kwa mabao 3-0 katika nusu fainali ya kombe hilo, na kuhitimisha safari ya Ubingwa wa FA kwa ushindi mwembamba iliyoupata baada ya kuilamba Portsmouth bao moja kwa sinia.

 

Hadi kufikia fainali, wababe hao wa Darajani waliwapiga Tottenham 5-1 na kutinga fainali na kubeba shaba baada ya kuifunga Liverpool 2-1.

 

Kwa rekodi hiyo, mashabiki wengi wanaipa timu hiyo ya Darajani nafasi kubwa ya kushinda Kombe hilo, pamoja na kuwa Matajiri hao wa London si wa kubeza kutokana na kuwa na rekodi nzuri katika ligi ya Barclays.

 

 

Please follow and like us:
Pin Share