Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

SHIRIKA la Vi agroforestry limeandaa kongamano la 11 la kitaifa la kilimomisitu linalotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 19 katika kituo cha mafunzo ya kilimomisitu, Bweri, musoma.

Meneja Mkazi wa shirika hilo, Martha Olotu alisema jana kuwa kongamano hilo limebeba kauli mbiu ya “kilimomisitu kwa vijana na uwekezaji”, kongamano linatarajiwa kuwakutanisha takribani washiriki 8,000 ana kwa ana.

Alisema washiriki wengine watashiriki kwa njia ya mtandao, ili kuharakisha upatikanaji wa fedha, kuimarisha ushirikiano na kuchochea utekelezaji wa hatua za vitendo katika sekta ya kilimomisitu.

“kongamano hili linalenga kubadili fursa za kilimomisitu kıva umekezaji unaotekelezeka, kuchochea fursa za kinchumi kwa vijana, kumarisha usalama wa chakula na kuchangia urejeshaji wa mandhari” alisema.

“tunawaalika serikali, wawekezaji, wadau wa maendeleo, watafiti, wakulima na vijana kujadili na kupanga utekelezaji wa pamoja, ” alisema martha olotu

“kwa kuzingatia zaidi ya miaka kumi ya majadiliano ya kitaifa na miongo minne ya utekelezaji wa kilimomisitu katika jamii, kongamano la 11 la kitaifa la kilimomisitu litaweka mkazo katika kuunganisha sera, uwekezaji na utekelezaji” alisema.

Aidha, alisema kongamano hilo litawakutanisha wadau kutoka serikalini, wakulima, watafiti, asasi za kiraia, taasisi za fedha, wadau wa maendeleo, wafanyabiashara na vijana ili kubadilishana uzoefu, kuimarisha ushirikiano na kukubaliana kuhusu hatua za vitendo za kupanua kilimomisitu nchini.

Alisema kongamano litatoa nafasi kwa wadau kutathmini maendeleo ya utekelezaji wa mkakati wa taifa wa kilimomisitu, kupitia maazimio ya kamati ya kitaifa ya ushauri kuhusu kilimomisitu na kukubaliana kuhusu hatua zinazohitaji kupewa kipaumbele.

Alisema pia watazindua jukwaa la wadau wa kilimomisitu tanzania (tanzania agroforestry stakeholders platform – tasp), litakaloimarisha uratibu wa wadau na kufuatilia uingizaji wa mapendekezo ya kongamano katika sera, mipango, bajeti na uwekezaji.

Alisema kongamano linatarajiwa kuwakutanisha takribani washiriki 8,000 ana kwa ana, pamoja na washiriki wengine kwa njia ya mtandao, ili kuharakisha upatikanaji wa fedha, kuimarisha ushirikiano na kuchochea utekelezaji wa hatua za vitendo katika sekta ya kilimomisitu

Alisema siku tatu za kongamano programu ya kongamano imejengwa katika maeneo matatu yanayokamilishana ambapo siku ya kwanza kutakuwa na fursa za biashara na uwekezaji wa kijani kwa vijana katika kilimomisitu.

“siku ya pili mchango wa kilimomisitu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuimarisha usalama wa chakula na kurejesha mandhari na siku ya tatu tutajadili uimarishaji wa utekelezaji wa sera za kilimomisitu” alisema.

Alisema mdahalo wa vijana utawakutanisha vijana na watunga sera, taasisi za fedha, wawekezaji, wakulima na wafanyabiashara ili kujadili vikwazo vinavyowakabili katika kupata mitaji, ardhi, masoko na huduma za

kitaalamu.

“kupitia majadiliano na uwasilishaji wa mawazo ya biashara, washiriki watabainisha fursa za biashara, changamoto za ufadhili na hatua za kutekeleza mapendekezo yatakayowasilishwa katika kikao cha kufunga kongamano,” alisema.

Aidha, alisema shughuli nyingine zitajumuisha vikao vya pamoja, mada za kitaalamu, maonesho ya ubunifu na biashara, mafunzo ya vitendo shambani, simulizi za wakulima, mijadala kuhusu uwekezaji na mikutano ya kuwaunganisha wafanyabiashara na washirika wenye fursa za kibiashara.

Alisema washiriki pia watajifunza kwa vitendo kuhusu mifumo mbalimbali ya kilimomisitu katika kituo cha mafunzo ya kilimomisitu, bweri, musoma