WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Ngoyai Loowassa ameeleza kusikitishwa kwake na kifo cha aliyekuwa mwanasiasa mkongwe nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, aliyefariki dunia jana Ijumaa, Feb. 2, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Akisaini kitabu cha maombolezo.

Akizungumza nyumbani kwa marehemu mara baada ya kuwasili, Lowassa amestuka na kusikitishwa sana musiba huo huku akisema si yeye tu bali taifa zima limeguswa kifo hicho.

“Mzee Kingunge alikuwa kiongozi wetu wa Chama Cha Mapinduzi kwa muda mrefu sana, nilifanya naye kazi nikiwa makao makuu ya chama na hata baada ya kutoka, alikuwa mtetezi wa sera za kijamaa. Tutamkusa mzee wetu. Mzee alikuwa muungwana sana, aliwaheshimu wote, hakuwahi kugombana na mtu na alifanya kazi na kila mtu.

“Nitaukumbuka moyo wake wa kusaidia watu na kushukuru watu, alikuwa jasiri sana. Hata pale ukipingana naye alisimama kushawaishi mpaka ukubali. Alikuwa anapenda kushawishi zaidi kuliko kulazimisha.

Mzee Kingunge alifariki jana, Februari 2 na anatarajiwa kuzikwa KESHOKUTWA Jumatatu, Februari 5, katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

ANGALIA VIDEO YA LOWASSA AKIWA MSIBANI KWA KINGUNGE

Please follow and like us:
Pin Share