Katika kuadhimisha siku ya Moyo Duniani tarehe 29/09/2023 yenye kauli mbiu “Tumia Moyo, Kulinda Moyo wako” wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Bingwa wa Moyo Tanzania (TCS) watatoa huduma ya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani.

Upimaji huu utafanyika katika viwanja vya Hospitali ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group iliyopo TAZARA wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam kwa siku mbili za tarehe 29/09/2023 na 30/09/2023 kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa 10 kamili jioni.

Kutakuwa na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora ambayo itawapa wananchi uelewa na kufuata mtindo bora wa maisha na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo ambayo yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa. Huduma hii itatolewa kwa watoto na watu wazima bila malipo yeyote yale.

By Jamhuri