Na Jumanne Magazi, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Efm na TV E, Fransis Siza (Majizo) amezindua , kampeni mbili za kuinua na kusaidia vijana nchini ili kupata fursa za ajira na kuibua vipaji vyao.

Ameyasema hayo,wakati alipokuwa akizindua kampeni hizo zitayokwenda kujulikana kama, Majizo Jobs Campaign na Kitaa Hubs.

Amesema lengo la kuanzisha mchakato huo ni kuwapa vijana sehemu maalum ya kuonyesha uwezo wao na vipaji walivyonavyo.

Majizo amesema kwa kuwa amekuwa akipokea jumbe nyingi kwenye mitandao zikimtaka kuwasaidia vijana ikiwemo kuwatafutia kazi huku idadi kuwa kubwa ameona ni bora kutengeneza jukwaa hilo.

Katika hatua nyingine majizo amesema wakati wakisheherekea miaka 10 tokea kuanzishwa kwa kampuni ya EFM,wamekuwa wakisaidia makundi maalum ikiwemo bodaboda,wajasiliamali, na vikundi vya sanaaa.

Majizo ameendelea kuweka wazi kuwa yeye na wadau wake wakaribu wameamua kuwapa vijana njia rahisi yahours kufikika ili watu watakao shida ya kupata wataaalam wa nyanja mbalimbali basi watakwenda kwenye jukwaa hilo

Majizo ambaye kitaaluma yeye ni DJ amesema kampeni hiyo itakuwa endelevu na kwa kuanzia watachukuwa vijana zaidi ya 150 na kuendelea.

Aidha amefafanua namna ya kujiunga na kampeni hiyo ya MAJIZO JOBS CAMPAIGHN ,pamoja na KITAA HUBS) ambapo kijana anatakiwa kuingia kwenye mitandao ili kuweza kujisajili tayari kwa kampeni hiyo.

Akizungumzia mafanikio ya kituo hicho amesema kwa kipindi cha miaka 10 wameweza kusaidia kuutambulisha muziki wa singeri na kuwawezesha vijana wa bodaboda ambapo wameweza kutambulika kama ajira rasmi.

Please follow and like us:
Pin Share