Na Jumanne Magazi, JamhuriMedia, Dar es Salaam

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, January Makamba amezindua kamati maalum itakayosimamia na kushughulikia chuo Cha uhusiano wa kimataifa Diplomasia cha Salim Ahmed Salim.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Machi 20, 2024, amesema kamati hiyo imepewa majukumu maalum ya kiutendaji ili kukihimarisha chuo hicho.

Makamba amesema wajumbe wa kamati walioteuliwa wanasifa na wabobezi katika nyanja ya diplomasia za kimataifa na pia wameitumikia Taifa katika nyadhifa mbalimbali nchini.

Aidha kamati hiyo yenye wajumbe saba huku mwenyekiti wake wao akiwa ni Balozi Khamis Kagasheki na makamo wake akiwa ni balozi Ramadhani Dau.

Wengine ni Profesa Masilina Chinoriga (mjumbe), Dk Salim Ali (mjumbe), Dk Singo (mjumbe), Ashumta Muna (mjumbe), Dk Shule (mjumbe), Dk Sanga (mjumbe)

Kazi za kamati: Makamba amezitaja kazi za kamati hiyo kuwa ni pamoja na kupendekeza muundo wa kisheria wa uongozi wa kituo

Kupendekeza aina ya mafunzo na mitaala ya chuo, Kamati inatakiwa kuwa na uwezo wa kubuni fikra za aina ya uongozi wa chuo, Kupendekeza muundo wa uombaji wa ajira kwa watu mishi na wafanyakazi wa chuo.

Kamati pia itakuwa na kazi ya kujua ni namna Gani chuo kitaweza kuiendesha ikiweno kubuni namna ya njia za kujipatia pesa za kujiendesha chenyewe.

Kamati pia imepewa kazi ya kutoa maoni na ushauri kwa wizara kwa jambo lolote ambalo litakuwa na tija kwa chuo.

Katika hatuna nyingine Makamba amekumbusha kuwa chuo cha uhusiano wa diplomasia cha salim Ahmed Salim ni moja ya chuo kikongwe barajni Afrika kilichojizolea sifa nyingi kutokana na kuzalisha viongozi wengi kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Wakati huo huo Makamba amezungumzia mafanikio ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia suluhu Hassan kuwa imekuwa na mafanikio makubwa katika kanyanja za diplomasia za kimataifa tokea aingie madarakani.

Aidha Makamba amesema uongozi wa Samia umeleta mafanikio makubwa ikiweno kuirudisha nchi kwenye majukwaa ya kimataifa na nchi imekuwa ukipata fursa nyingi za kiuchumi na kijamii.

Naye mwenyekiti wa kamati hiyo Balozi Khamis kagasheki kwa upande wake amemshukuru mheshimiwa Waziri Makamba na kamati yake kwa uteuzi wake na Imani kubwa waliyonayo kwake.

Aidha balozi kagasheki ameitaka kamati hiyo kufanyakazi kwa nguvu moyo, ueledi,kijituma Uzalendo kwa Taifa kwani wao ni kati ya watanzania wengi waliopata bahati ya kuitumikia kamati hiyo.

Kwa upande mwingine kagasheki ameomba wadau pamoja na serikali kunisaidia kamati hiyo ILI kuifikia malengo na mikakati waliopewa kuyatekeleza,pia amempongeza mh RAIS Samia kwa kutimiza miaka mitatu ya uongozi wake nakusema watanzania Bado wanimani kubwa na serikali yake.

By Jamhuri