
Mama Maria Nyerere akizungumza wakati alipokutana na waendesha baiskeli wa msafara wa Nyerere Cycling Tour ambapo Vodacom Tanzania Plc waliokwenda kumuaga na kupata baraka zake kabla ya kufanya mashindano ya Vodacom Coastal Classic pamoja na Nyerere Cycling Tour.
Safari ya Nyerere Cycling Tour kutoka Dar es Salaam hadi Butiama, mkoani Mara, inalenga kumuenzi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa kuunganisha mchezo wa baiskeli na jitihada za kuleta matokeo chanya katika jamii.
Kupitia safari hiyo, waandaaji na washirika wanatarajia kutekeleza shughuli mbalimbali zinazogusa elimu, afya, uhifadhi wa mazingira, elimu ya fedha na maendeleo ya jamii zikiwemo utoaji wa madawati 1,000, ujenzi wa madarasa 10, ukarabati wa madarasa 40 na upandaji miti, huku shughuli hizo zikitarajiwa kuwafikia zaidi ya watu 25,000.
Tukio hilo lilishuhudiwa na Meneja mauzo na mkakati wa biashara wa kanda ya Dar es salaam na Pwani Vodacom Tanzania PLC Caleb Majo(kulia), mtoto wa Mwalimu Nyerere – Madaraka Nyerere (wa pili kushoto) na Wilmot Ishengoma, Mkuu wa Kitengo cha Tahadhari wa Stanbic Bank Tanzania (kushoto) pamoja na wadau wengine wa mchezo wa baiskeli.
Tukio hilo lilifanyika wikendi hii, jijini Dar es salaam.







