Wanachama wa Nato wanafikiria kuisaidia Ukraine silaha zaidi na risasi kwa ajili ya kuendelea kujilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi. 

Nchi ya Marekani imekuwa mstari wa mbele kutoa msaada mkubwa wa kijeshi kwa Ukraine, ambapo imetangaza tena kuwapa msaada mpya wa kijeshi wenye thamani ya dola milioni 500.

Marekani pia imethibitisha kuwa itatoa silaha za cluster, uamuzi ambao umeleta utata na kusababisha wasiwasi miongoni mwa washirika wa Nato.Ukraine pia itapokea makombora kutoka Ufaransa – sawa na makombora ya Uingereza Storm Shadows ambayo yalitolewa hivi karibuni.

Aidha Kuna ahadi ya kutolewa dazeni ya vifaru, ambapo Ukraine wamesema wanahitaji kulinda eneo lake na kuwaondoa wanajeshi wa Urusi hivyo nchi zote wanachama watatuma vifaru vya idadi tofauti wakiongozwa na.

Vifaru vya Leopard 2 hutumiwa na nchi nyingi za Ulaya, na vinaelezwa ni rahisi kuvitunza na havitumii mafuta mengi kama vifaru vingine.

Katika miezi ya kwanza baada ya uvamizi huo, Nato ilipendekeza nchi wanachama kuwasambazia Ukraine vifaru. 

Wanajeshi wa Ukraine wanajua jinsi ya kuviendesha, na jinsi ya kuvitunza, na walikuwa na vipuri vya kutosha.

Vifaru vingi vya kisasa vya Magharibi ni vigumu kuvitumia na kuvitunza. Picha za hivi karibuni za shambulio la Ukraine kwenye himaya za Urusi zinaonyesha vifaru vya Leopard na Bradley tayari vinatumiwa na vikosi vya Ukraine.

Uingereza ilikuwa ya kwanza katika Nato kutoa kifaru cha Challenger 2. Ambacho  kiliundwa miaka ya 1990 na Ndio kifaru bora zaidi miongoni wa vifaru vinavyotumiwa na vikosi vya Ukraine. 

Tangu Februari 2022 Ukraine tayari wamepokea zaidi ya vifaru 200 aina ya T-72s, kutoka Poland, Jamhuri ya Czech na nchi nyingine. Akitangaza uamuzi wa Marekani wa kutuma vifaru 31 vya Abrams nchini Ukraine, Rais Joe Biden alivitaja kuwa 

“vifaru vyenye uwezo mkubwa zaidi duniani.” Huku akitoa ahadi ya Marekani kuanza  kuwafunza wanajeshi wa Ukraine namna bora ya  kuvitumia lakini bado haijafahamika itachukua muda gani hadi vifaru vyenyewe kuwasili

By Jamhuri