Jeshi la wapiganaji la Rapid Support Forces (RSF) limefanikiwa kumiliki Darfur Kusini huku kukiwa na taarifa zaidi za ukiukwaji wa haki za binadamu.

Mapigano kati ya RSF na Jeshi la Sudan yamefanya familia kadhaa kuvunjika na kukosa makazi.

Zipo taarifa kuwa wapiganaji wa RSF pia waliharibu na kuvunja majengo ya serikali na masoko.

Tangu kuanza kwa vita hiyo katikati ya Aprili mwaka huu, watu wasio na asili ya Kiarabu katika maeneo mbalimbali ya Darfur wamekuwa waathirika kutoka kwa RSF na washirika wao.

Mapigano ya nguvu yameendelea Khartoum ambao ni Mji Mkuu wa Sudan, na maeneo ya karibu. Taasisi za kimataifa zinaendelea na upatanishi kumaliza mgogoro huo.

Vita kama hiyo ilitokea miongo miwili iliyopita ambapo jeshi lilipambana na waasi. Watu 300,000 walikufa kwenye vita hiyo.