Na Richard Mrusha, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema mkutano wa wakandarasi uliofanyika jijini Dar es Salaam umekuwa na tija kubwa na wakihistoria na ni jambo ambalo halijatokea nchi nyingine yeyote Afrika bali Tanzania hivyo, hiyo ni heshima kubwa .

Amesema kuwa ni heshima kubwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo wa wakandarasi wanaojiuhusisha na uchimbaji wa madini chini ya bahari ni jambo jipya ambalo kama Tanzania imekuwa ni fursa pekee ya kujifunza na kuelewa rasilimali zilizopo duniani na namna ya kuweza kuzivuna ili kuongeza mapato.

Mavunde ameyasema hayo leo Oktoba 24, 2023 jijini Dar es Salaam ambapo Tanzania imepata heshima hiyo yakuwa nchi mwenyeji wa mkutano wa sita wa wakandarasi na kwamba zipo fursa zingine zinaweza kuongeza uchumi wetu kupitia madini ya uchumi wa bahari.

“Hivi sasa dunia inakwenda katika madini ya mkakati ambayo yanasaidia sana katika nishati safi na mwelekeo wa dunia ni kwamba ikifikapo 2050 kuachana na nishati ambayo inachafua mazingira ambayo na hali ya hewa iliyoko chini ya bahari ambapo kwa asilimia kubwa ni yale ambayo yanakwenda kushghulikia upatikanaji wa nishati safi “amesema Mavunde.

“Kama Tanzania imekuwa muda wote sehemu nzuri ya sisi kuweza kujifunza na kubadilishana uzoefu na wenzetu ikiwa ni namna bora ya kuweza kushiriki katika uvunaji wa madini ya chini ya bahari na naamini kwamba hii itakuwa ni fursa kubwa na fursa ya kipekee ya kuongeza uchumi wetu wa madini katika nchi yetu ya Tanzania.

Nakuongeza kuwa kwa sababu tumeanza mwanzo huu mzuri wa sisi kuwa wenyeji hivyo tunaamini kwa ushirikiano ambao tumeupata kutoka kwa hawa wenzetu ambao wamefika hapa itakuwa ni njia ya kwanza kuifanya Tanzania kunufaika na madini chini ya bahari “amesema.

Mavunde ameongeza kuwa ni fursa ya kipekee na kubwa kama nchi tumeichukua na kwa uzito mkubwa na tutaangalia namna ya utekelezaji wake sisi kama ni wanachama wa hii mamlaka ya madini ya bahari na kama Tanzania pia tunayo nafasi ya kushirki moja Kwa moja kwenye uchumi huu na tupo tayari kulifanya jambo hilo “amesema.

Pia Waziri Mavunde ameongeza kuwa katika mkutano huo wa siku tatu wa wakandarasi jambo kubwa ambalo wametokana nalo ni kwamba wamepata fursa ya kupata uelewa wa kutosha juu ya madini yaliyopo chini ya bahari ambapo kwa kiasi kikubwa yana mchango mkubwa kwenye nishati safi ambayo ndio mwelekeo wa kidunia.

Amesema kuwa mkutano huo umesaidia kuweka mikakati na kuweka mipango mizuri ya kuhakikisha kwamba Tanzania inanufaika na madini ya chini ya bahari lakini jambo la pili ni lini tutaanza utekelezaji huo kama alivyosema kuwa Tanzania ni mwanachama wa ISA.

Amefafanua kuwa mkutano huo unamaana kubwa sana kwa Tanzania kwa sababu mambo makubwa mawili ya kwanza umeitambulisha Tanzania katika ulimwengu wa sekta ya madini kwa sababu kwa Afrika Tanzania ndio nchi ya kwanza kuwa mwenyeji wa mkutano huo hivyo imekuwa sehemu ya Kuitangaza Tanzania.

Pia jambo la pili ambalo ni kubwa ni kwamba imepatikanika nafasi ya kuelewa zaidi na kupata uzoefu na wenzetu ambao wanauelewa mkubwa na maendeleo makubwa katika jambo hilo hivyo Tanzania imepata nafasi ya kuwa katika timu ya hatua za awali za kushiriki ili kuweza kuongeza uelewa hasa wadau kutoka katika Wizara ya Madini hivyo sio mkutano wa bure ni mkutano ambao unaacha ujuzi unaokwenda kuwajengea uwezo wa Tanzania katika kufikia uchumi wa bahari.

” Kwa ujumla kama nchi tunao mwelekeo wa hivi sasa kuja na mkakati wa kuyavuna madini ya kimkakati ambayo kwa mahitaji ya Leo duniani zaidi ya tani milioni 10 zinahitajika Kwa ajili ya,madini haya ya kimkakati na ikifika mwaka 2050 mahitaji yatakuwa tani milioni 150 kama Tanzania ni wakati muafaka sasa wa kuaza mikakati kupitia uvunaji wa rasilimali hiyo katika uchumi wa bahari na kuweza kufikia uchumi huo wa bluu ifikapo mwaka 2050.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Same Mjini, David Mathayo ambaye alihudhuria kilele cha mkutano huo amesema kuwa katika Afrika Tanzania ndio nchi ya kwanza kuongea na wadau hao ambao wanafanyakazi ya kutafiti na kuchimba madini yaliyopo chini ya bahari

Amesema kuwa sasa hivi tunakabiliwa na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yanatokana na matumizi ya nishati ambazo zinatoa Cabondioxide na kusababisha upungufu wa hewa safi na ongezeko la joto duniani hivyo panapotokea kuwepo na utafiti wa kuashiria kubainisha nguvu za umeme wa madini.

By Jamhuri