Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Manyara

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara Yustina Rahhi ameandaa mafunzo ya ujasiriamali kwa wajengea uwezo akina mama na vijana wajasiriamali wa Mkoa wa Manyara ili kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kupelekea uchumi wa kati.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Rahhi amesema mafunzo hayo kimkoa yameanzia Wilaya ya Mbulu tangu Mei 20 hadi Juni 28 mwaka huu 2024 yatakapomaliza mkoani humo.

Mbunge Rahhi amesema walengwa wa mafunzo hayo ni akina mama wajasiriamali wote kuanzia ngazi za matawi hadi Wilaya wakiwemo viongozi mbalimbali kama madiwani wa Viti Maalum, madiwani wa Kata wanawake, na viongozi wa UWT ngazi ya matawi hadi Wilaya.

” Kwa Wilaya ya Kiteto, mafunzo haya yatatolewa kuanzia Juni 24 hadi Juni 28, kuanzia saa mbili asubuhi na kumalizika saa name mchana katika ukumbi wa Kauli Njema ( TESHA ) amesema Mh.Rahhi.

Aidha Mh. Rahhi ametaja Mada mbalimbali zitakazofundishwa Kwa wajasiriamali hao kuwa ni pamoja na Ufugaji kibiashara, Kilimo Biashara, Batiki aina zote, Sabuni aina zote, Keki Pili pili kali, Karanga, Tambi, Utafutaji wa masoko, na usimamizi wa Biashara.

” Wilaya ya Mbulu,mkila Halmashauri baada ya mafunzo, Mbunge Rahhi aliwezesha kutoa vifaranga 4000 kila Halmashauri, Hanang pia ametoa vifaranga 4000, baada ya mafunzo hayo Mbunge Rahhi atawezesha kutoa mtaji wa vifaranga vya kuku vipatavyo 4000 kwa washiiriki wote wa mafunzo ya Uuasiriamali watakaokuwepo wilayani Kiteto, amesema Rahhi.

Hata hivyo amewataka akina mama hao wajasiriamali kuhakikisha wanahudhuria mafunzo hayo kikamilifu ili kuweza kutoka hapo wakiwa na elimu nzuri na kubwa ya ujasiri na hatimaye waweze kujikwamua kiuchumi na na umaskini.