Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia, Dodoma

Muelekeo wa Sekta ya Madini unalenga Katika kuhakikisha mchango wa sekta ya Madini Katika Pato la Taifa unafikia asilimia 10 na zaidi Ifikapo mwaka 2025 kama inavyofafafanuliwa Katika Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Madini wa Mwaka 2019/2020_2023/2023.

Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Time ya Madini Mhandisi Ramadhan Lwamo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Time ya Madini kwa Kipindi Mwaka 2022/2023 na mikakati ya Mwaka 2023/2024.

Amesema Katika kuhakikisha azma hiyo inafikiwa ,tume ya Madini inatarajia kuwa na mikakati Maalumu ili kuwa na shughuli za Madini ambazo ni endelevu kwa kuimarisha Usimamizi na udhibiti Katika Maeneo ya uzalishaji wa Madini ujenzi na Madini ya viwandani kwa kuongeza wakaguzi wasaidizi wa madini ujenzi (AMAs).

“Kuwa na vitendea kazi (PoS) pamoja na kushirikisha Mamlaka nyingine za serikali zinazosimamia na kutumia rasilimali hizi (Halmashauri,polisi,TARURA na TANROADS),” Amesema Kaimu Katibu Mtendaji huyo.

Na kuongeza ” Kuimarisha udhibiti wa biashara haramu ya Madini, uboreshaji na Usimamizi thabiti was Mfumo was utoaji wa lesen za Madini, kuimarisha ukaguzi Katika shughuli za uchimbaji migodini,Kufungua na kuimarisha Ofisi mpya, kuimarisha shughuli za tafiti, kuimarisha masoko ya Madini yalipo mipakani ya nchi kuimarisha Mazingira ya uwekezaji,” Amesema Lwamo.

CHANGAMOTO

Amesema pamoja na mafanikio makubwa ya Sekta ya Madini yaliopatikana kutokana na kuanzishwa kwa time ya Madini zipo Changamoto ambazo ni uelewa Mdogo was sheria ya Madini ya Sura ya 123 na kanuni zake kwa wachimbaji na wafanyabishara wa Madini na Umma kwa ujumla hivyo kusababisha uwepo wa migogoro ya Mara kwa Mara .

MIKAKATI YA UTATUZI WA CHANGAMOTO HIZO.

Ameeleza ni pamoja na Kuendelea kutoq elimu ya sheria ya Madini pamoja na kuendesha Mafunzo ya Mara kwa Mara Katika Maeneo ya wachimbaji wadogo na viongozi wa serikali za mitaa ili Kujenga uelewa wa Sheria hiyo na kupunguza migogoro baina ya wachimbaji.