Bodi ya Ligi (TPLB) imefanya mabadiliko ya mchezo namba 153 kati ya Lipuli na Ndanda uliokuwa uchezwe Ijumaa Machi 2, 2018 kwenye Uwanja wa Samora,Iringa.

Mchezo huo wa raundi ya 20 ligi kuu soka Tanzania Bara sasa umesogezwa mpaka Jumapili Machi 4, 2018 na utachezwa kwenye Uwanja ule ule wa Samora mkoani Iringa.

Bodi imeeleza sababu za kusogezwa mbele kwa mchezo huo ni kuipa nafasi Ndanda FC kusafiri kutoka Mtwara hadi Iringa baada ya mchezo wao wa kiporo dhidi ya Yanga.

Mchezo wa Ndanda FC na Yanga wenyewe umepangwa kuchezwa Jumatano Februari 28, 2018 kwenye Uwanja wa Nangwana Sijaona, mkoani Mtwara.