MKUU wa Majeshi yaUlinzi nchini (JWT), Venance Salvatory Mabeyo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wameongoza maadhimisho ya mwaka wa 54 tangu kuundwa kwa jeshi hilo, kwa kufanya usafi jijini Dar es Salaam.

Mabeyo na Makonda mapema leo wamefanya usafi katika eneo la Kambi ya JWTZ eno la Lugalo jijini Dar es Salam sambamba na viongozi mbalimbali wa jeshi hilo.

Akizungumza mara baada ya zoezi hilo, Jenerali Mabeyo amesema jeshi lake lipo imara na litahakikisha amani na utulivu vinatawala katika taifa na hivyo wananchi waendelee kuliamini jeshi hilo.

Kwa upande wake Paul Makonda, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya jeshi hilo vilivyopo Mwenge, amelipongeza jeshi hilo kwa ukakamavu wake hasa kwa namna ambavyo lilipita mbele likionyesha namna linavyoweza kufanya kazi yake kupitia mbwa wenye mafunzo maalum na kuahidi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo katika shughuli mbalimbali hasa za kijamii.

Please follow and like us:
Pin Share