Na Dotto Kwilasa,JamhuriMedia, Dodoma

Ndani ya kipindi cha miaka 60 ya Muungano ,Serikali imefanya uboreshaji mkubwa wa Ofisi na Makazi ya askari wa Vyombo vya Usalama vya Muungano na kubadilisha mfumo wa ujenzi wa nyumba za askari wa vyeo mbalimbali kutoka kuwa nyumba za mabati na kuwa nyumba za kisasa.

Imeelezwa kuwa hadi sasa Jeshi la Polisi limejenga nyumba ni 10,450 kwa ajili ya makazi ya askari wake. Pia zimejengwa Zahanati za Jeshi la Polisi 35 katika Mikoa mbalimbali nchini ambazo huduma za matibabu kwa askari wa Jeshi la Polisi, familia zao na raia wa kawaida.

Hayo yamesemwa Jijini hapa na
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamadi Masauni wakati wa mikutano wake na waandishi wa habari ambapo amefafanua kuwa kwa upande wa Idara ya Uhamiaji Serikali imeiwezesha kujenga nyumba 454 kwa ajili ya makazi ya Maafisa, Askari na watumishi wake katika Mikoa mbalimbali nchini, ukilinganisha na majengo machache ya Makazi yaliyokuwepo kabla ya Muungano mwaka 1964.

“Ujenzi wa makazi ya Askari umesaidia kuwaweka sehemu moja na kuwa rahisi kupatikana kwa haraka pale wanapohitajika kwa dharura. Pia, umesaidia kupunguza gharama kwa askari ya kupanga uraiani na kuongeza usalama zaidi kwa askari, ” Amesema Mhandisi ,Waziri Masauni

Amesema Katika kipindi cha miaka 60 ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania, Jeshi la Polisi limefanikiwa kujenga Vituo vya Polisi 485 vya daraja ‘A’, ‘B’ na ‘C’ pamoja na ofisi 20 za Makamanda wa Polisi katika Mikoa mbalimbali nchini.

“Ujenzi wa Vituo vya Polisi umesaidia kusogeza huduma za polisi kwa wananchi na kuwafanya wananchi kupata fursa ya kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwani zamani huduma hizo walikuwa wanazipata kwa kutembea umbali mrefu na kuwafanya kubaki na taarifa za matukio waliyosikia au kuona kutokana na kushindwa kuyafikisha kwenye Kituo cha Polisi kwa kuhofia kutembea umbali mrefu kwenda kutoa taarifa, “ameeleza

Please follow and like us:
Pin Share