Na Magrethy Katengu, Jamuhuri media
Dar es Salaam

Kanisa la Assembles of God(TAG) kwa kushirikiana na SOS Adventure wanatarajia kubadilisha wale wote waliofungwa na kamba za shetani kwa kutoa mahubiri, kufanya maombi kwa Mungu ili wawekwe huru katika Kristo Yesu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 8,2024 Jijini Dar es Salaam Johannes Amirzer Mwinjilisti kutoka Australia ambaye ndiye Muhubiri Mkuu katika mlipuko wa Tamasha la furaha litakaloanza hapo kesho Julai 9hadi 14 mwaka huu katika viwanja vya Mwembeyanga Temeke ambapo amesema siku hizo zote kutakuwa na maombi na Mungu ataponya walio na magonjwa ,na wafanyabiashara wataombewa .

“Katika tamasha hilo kutakuwa na timu ya watu 250 kutoka nchi tofauti tofauti wataungana na wakazi wa Dar es Salaam kutoka dini zote watu zaidi ya 2000 wakihubiri Upendo wenye nguvu ya Yesu Kristo na waraibu wa dawa za kulevya walioshindikana tunawakaribisha,makahaba,kwani tutafanya maombi kwa ajili yao na Mungu atawabadilisha kuwafanya kuwa wapya ikiwa jamii ilikuwa imewatenga watawasaidia “amesema Mwinjilisti Amirzer.

Mwinjilisti amesema kuwa tamasha hilo maandalilizi yake hadi kuhitimisha limegharimu kiasi cha shilingi bilion 1 na milioni 200 kwani kutakuwa na semina zitakazotolewa katika uwanja wa uhuru kwa vijana pia watafanya maombi kwa ajili ya kuombea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kuanza mwaka huu ili Mungu aendelee kushikilia amani iliyopo kusitokee machafuko yeyote na wataombea viongozi wote wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Mungu aendelee kumpa hekima maarifa na busara katika kuliongoza Taifa.

Sanjari na hayo amesema amesikitishwa sana na tulio lililotukia hivi karibuni mauaji ya Albino hivyo hivyo anaamini kitendo hiko kilichofanyika kinahusishwa na nguvu za kishirikiana waganga wa kienyeji hivyo maombi yatafanyika wale wote waliohusika Mungu atawashushia laana kwani kundi hilo la maalibino kuzaliwa katika nchi yeyote ni Baraka kwa Taifa na wanaowauwa wanatenda dhambi kubwa

Aidha katika Tamasha hilo Rais Dkt Samia amealikwa kuhudhuria kufungua kwani ni sherehe kubwa za miaka 85 ya tangu kuanzishwa kanisa la TAG na hivyo mahubiri yatakayofanyika Mwinjilisti Johannes atatumia muziki, video na mazungumzo yaliyoonyeshwa kuwasilisha neno la Mungu ujumbe wa amani na matumaini.

Sambamba na yote hayo SOS adventure inajivunia kuwepo kwa waimbaji wa nyimbo za injili Rose Muhando,Boazi Danken, Julia Willander kutoka Kenya na waimbaji wengine watakuwepo wakiimba wakati wa usiku wa tamasha hilo hivyo kila Mkazi wa Dar es salaam asikose kuhudhuria