Miaka tisa tokea dunia ipate taarifa za kifo cha mfalme wa muziki wa
Pop duniani Marehemu Michael Jackson ambaye alifahamika
duniani kote kutokana na upekee aliokuwa nao katika uchezaji
pamoja na nyimbo zake ambazo zilipendwa na watu wengi
ulimwenguni.
Marehemu Michael Jackson alipendwa zaidi na watoto kutokana na
upendo na ukaribu aliokuwa nao kwa watoto wote ambapo hakujali
rangi na enzi za uhai wake Michael Jackson aliwahi pia kutembelea
Tanzania na kukutana na Rais wa awamu ya pili wa Tanzania
mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
Marehemu Michael Jackson alifariki June 25,2009 akiwa nyumbani
kwake Holmby Hills, Los Angeles nchini Marekani ambapo alikutwa
chumbani kwake na mmoja wa madaktari wake Conrad
Murray akiwa hapumui na kukimbizwa hospitali ya Ronald
Reagan UCLA Medical Centre.
Marehemu Michael Jackson aliwahi kushinda tuzo ya Grammy
Awards katika wimbo bora wa RnB mwaka 1984, Grammy Award
wimbo bora wa mwaka 1986, MTV video music award 1995,Billboard
Music Award for spotlight 1989 na nyingine nyingi.
Marehemu Michael Jackson alitamba na ngoma kali ikiwemo
Thriller, Bill Jean, We are the World, The way you make me feel, Beat
It, You Rock My World, Earth song, Dirty Diana na nyingine nyingi
ambazo bado zinaheshimika duniani kote mpaka leo.

By Jamhuri