Kijana mmoja raia wa Somalia ambaye alioa wanawake wawili usiku mmoja amesema kwamba atawashawishi wanaume wengine kufanya hivyo.

Bashir Mohamed anasema kuwa aliwachumbia wanawake wote kwa takriban miezi minane na kuwashawishi kufunga ndoa naye.

”Nilikuwa nikiwaleta nyumbaji wote pamoja”, alisema.

”Nilikuwa nikiwaambia wazi wote wawili kwamba nawapenda. Waliridhika” , aliongezea.

”Umuhimu wa kuwaoa wote wawili wakati mmoja ni kwamba hawangekuwa na wivu na kwamba watajua tangu awali kwamba wamekuwa katika ndoa za uke wenza”, alisema bwana Mohammed.

Alioa wanawake wawili kwa sababu alihitaji watoto wengi.

”Nitawashawishi wanaume wengi pia kufuata nyayo zangu iwapo wana uwezo”, alisema Mohamed.

Ndoa za wake wengi ni halali katika utamaduni nchini Somalia lakini sio jambo la kawaida kuoa wanawake wawili wakati mmoja, kulingana na mwandishi wa BBC Mohamed Mohamed.

”Imetokea mara kadhaa katika miaka ya nyuma , ikiashiria kwamba huenda sasa ikawa mtindo mpya”, aliongezea.

Bwana Mohamed aliwaoa wanawake hao wawili , Iqra na Nimo, katika kijiji cha Sinai katika jimbo lililojitenga la Somaliland mnamo tarehe 22 mwezi Juni.

Please follow and like us:
Pin Share