Wanachama na wapenzi wa Klabu ya Soka ya Simba ya Dar es Salaam, pamoja na wapenzi wa soka ndani na nje ya nchi wako kwenye majonzi makubwa baada ya kutekwa kwa mfadhili na mwekezaji mkuu wa klabu hiyo, Mohammed Dewji (Mo).

Tangu taarifa za kutekwa kwake zianze kuvuma asubuhi ya Oktoba 11, mwaka huu, wanachama na wapenzi wa Simba wamekuwa wakikusanyika klabuni hapo Mtaa wa Msimbazi, wakiwa wenye majonzi.

Baadhi ya wazee wa klabu hiyo na wapenzi wa soka wameshiriki na wanaendelea kuomba dua ili Mo apatikane akiwa hai.

Mo anaheshimika kwa mchango wake mkubwa katika kuboresha maendeleo ya soka ndani ya Simba na timu ya taifa. Pichani, akiwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwenye maadhimisho ya Simba Day, Agosti 8, mwaka huu.

Please follow and like us:
Pin Share