Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Zanzibar

Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo amefanikiwa Kuubakisha mkanda wa WBO Afrika nchini kwa kumchapa ‘KO’ mwanajeshi wa Ghana, Elvis Ahorgah..

Mwakinyo ambaye amecheza Usiku wa Kuamkia Leo Visiwani Zanzibar, ameibuka na ushindi huo baada ya mghana kumuomba refa amalize pambano Raundi ya saba baada ya kuzidiwa….

Katika pambano Hilo la ‘Mtata Mtatuzi’ Bondia Hussein Itaba Nae ameshinda mkanda wa PST kwa Kumtwanga kwa pointi Juma Misumari.

Aidha Ali Mkojani Ameweka heshima nyumbani kwao Zanzibar kwa kushinda mkanda wa PST dhidi ya Juma Kijo wa Dar es Salaam…..