Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Naibu Waziri wa Maliasili wa China Sun Shuxian na ujumbe wake Ikulu Zanzibar tarehe: 28 Januari 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi ameishukuru Serikali ya China kwa misaada ambayo wamekuwa wakiipatia Zanzibar katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kudumisha uhusiano wa muda mrefu.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amesema China na Zanzibar zitatiliana saini hati ya ushirikiano katika sekta ya uchumi wa buluu ikiwemo sayansi na teknolojia ya baharini, uchunguzi wa mazingira ya bahari, utabiri wa ufuatiliaji na tahtmini ya maafa , utafiti wa baharini, kujengea uwezo, uwekezaji, uhifadhi wa viumbe hai wa baharini na ulinzi wa mfumo wa ikolojia wa baharini.

Naye , Naibu Waziri wa Maliasili wa China Mhe.Sun Shuxian ameeleza kuwa China inatoa fursa za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Kizanzibari katika fani ya bahari na viumbe wa baharini pia itaendeleza ushirikiano na Zanzibar .