Mwanasiasa wa cheo cha juu kwenye muungano wa upinzani nchini Zimbabwe MDC Tendai Biti amenyimwa hifadhi kwenye taifa jirani la Zambia.

Polisi wa Zimbabwe wanamlaumu Bw Biti kwa kuchochea ghasia kufuatia uchaguzi wa mwezi uliopita.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Zambia Joe Malanji aliiambia BBC kuwa vigezo vya vyake kuomba hifadhi vilikuwa dhaifu.

Alizuiwa eneo salama hadi pale aliporejeshwa Zimabwe, waziri alisema.

Mapema wakili wake alisema mteja wake alikuwa amezuiwa kwenye mpaka na Zambia na mamlaka za Zimbabwe.

Ripoti zingine za polisi wa Zambia zinazo sambaa kwenye mitandao ya kijamii zinasema kuwa maafisa wa Zimbabwe walijaribu kumkamata Bw Biti baada ya yeye kuvuka na kuingia Zambia.

Mwanasiasa huyo wa upinzani akaomba msaada kwa sauti na karibu ya wasafiri 300 wa Zimbabwe wakawazuia maafisa wa usalama wa seriali kumkamata, kulingana na ripoti.

Maafisa wa Zambia kisha wakaingilia kati na kutishia kuwakamata maafisa wa Zimbabwe kwa kujaribu kutekeleza wajibu wao ndani ya ardhi ya Zambia.

Please follow and like us:
Pin Share