Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akisalimiana na Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally, walipokutana Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Abeid Amani Karume. Dk. Nchimbi amewasili Zanzibar leo Jumamosi, Machi 2, 2024, akitokea nchini India, ambako amelazimika kukatisha ziara yake ya kikazi, kushiriki msiba wa Mwenyekiti wa CCM Mstaafu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu wa Awamu ya Pili, Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi.