Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia

SHIRIKA la Taifa la Maendeleo (NDC)limesema ndani ya kipindi cha mwaka mmoja linajivunia maendeleo yake kwa kufanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi ambayo imekuwa ikigusa sekta muhimu za kilimo, viwanda, madini, nishati pamoja na miundombinu ya biashara.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam jMkurugenzi Mtendaji wa NDC, Dkt Nicolaus Shombe wakati akizungumzia mafanikio ya Utekelezajib waliyoyapata ndani ya kipindi cha mwaka 2023/24 na matarajio yao miaka ya ijayo kupiga hatua kubwa zaidi ndani na nje ya nchi .

Sanjari na hayo Shirika la NDC tangu kunzishwa kwake ni kiota cha kutotolesha viwanda nchini kwani ndani ya mwaka mmmoja kufuatia mageuzi na mabadiliko mbalimbali yaliofanywa ikiwemo kusimamia miradi nane ya viwanda mama.

“Kwa kuzingatia heshima, juhudi na nia ya dhati ya Serikali yetu chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kujenga uchumi imara usio tegemezi, Shirika la Taifa maendeleo liko nae bega kwa bega likifanya kazi kwa uadilifu na ubunifu mkubwa”amesema.

Dkt Shombe amesema NDC limeendelea kufanikisha maono kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na huku wakiingia mikataba na wawekezaji katika sekta ya madini miradi ikiwemo Makaa ya mawe kuweza kufanikisha masuala mbalimbali kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi pamoja na kuinua sekta ya viwanda na uwekezaji Nchini.

Akitaja mafanikio hayo katika kipindi Cha mwaka mmoja ni pamoja na utekelezaji wa mradi wa kielelezo wa liganga na mchuchuma ambao uko katika wilaya ludewa katika mkoa wa Njombe ambao ulikabidhiwa kwa NDC mwaka 1996 .

Amesema mradi huo ni tofauti na miradi mingine kutokana na kuwa mradi unganishi kwani umekuwa unatekelezwa kwa pamoja kutegemeana.

Dkt Shombe amesema jumla ya tani 315,000 za makaa ya mawe zinatarajiwa kuchimbwa katika mwaka wa fedha 2023/24 katika mradi wa mchuchuma na kulipa ada ya mwaka Kwa leseni mdogo za uchimbaji nje ya leseni kubwa katika mradi huo.

“Huu ni moja ya miradi ya kimkakati na kielelezo iliyobainishwa katika dira ya taifa ya mwaka 2025,ilani ya CCM na Mpango wa tatu wa maendeleo wa miaka mitano”alisema

Hata hivyo amesema Shirika hilo limefanikiwa kulipa fidia ya jumla ya Billioni 15, 424, 364,900 kwa wananchi wanaopisha utekelezaji wa mradi wa Mchuchuma na Liganga.

Dkt Shombe amesema mradi mwingine ni wa magadi soda ambao uko monduli katika mkoa wa Arusha ambapo kupitia mradi huo Shirika limeendelea na hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata ofa ya leseni ya uchimbaji badala ya leseni 29 za awali .

“Katika mwaka wa fedha 2023/24 Shirika la Taifa la Maendeleo linatarajia kulipa leseni za uchimbaji ili kuruhusiwa kuendelea na hatua nyingine katika utekelezaji wa mradi pamoja na kulipa fidia wananchi watakaopisha mradi ili kuendelea na hatua nyingine ya utekelezaji wa mradi”alisema

Aidha Dkt Shombe amesema katika kusimamia kilimo cha mazao ya kimkakati ikiwemo zao la mpira kupitia mashamba ya mpira inayoyamiliko na yako kalunga katika mkoa wa morogoro pamoja na shamba la kihuhwi lililopo muheza katika mkoa wa Tanga..

Aidha NDC inatarajia kuzindua bidhaa mpya vviatilifu vya mazao na mbolea hii. ni kusaidia kipunguza kuagiza bidhaa nje ya nchi