Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

NMB Bank imejiunga kwa mara ya kwanza kuwa mdhamini wa Mbio za Mbuzi za mwaka 2026, zinazolenga kukusanya Sh milioni 200 kwa ajili ya kusaidia vijana 150 kujiunga na vyuo vikuu na mafunzo ya ufundi. Tukio hilo litafanyika Septemba 19 katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Wateja Maalum wa NMB Bank, Getrude , amesema uamuzi huo umetokana na uzoefu wa benki hiyo kama mshiriki wa tukio la mwaka jana pamoja na ulinganifu uliopo kati ya malengo ya Rotary na uwekezaji wa NMB katika elimu.

NMB hutenga asilimia moja ya faida baada ya kodi kila mwaka kwa uwekezaji wa kijamii. Mwaka 2025, benki hiyo ilitoa madawati 6,365 kwa shule 124 nchini, hatua iliyonufaisha takribani wanafunzi 19,095.

Rais wa Rotary Club of Dar es Salaam Oysterbay, Paul Muhato, amesema Sh milioni 163 kati ya Sh milioni 167 zilizokusanywa mwaka jana zimesaidia wanafunzi 136, wakiwemo 100 waliojiunga na vyuo vikuu na 36 waliojiunga na mafunzo ya ufundi.