Baadhi ya wanafunzi kutoka shule ya  msingi Nangombo na Limbo wakipokea msaada wa vifaa vya ujenzi  vilivyotolewwea na Benki ya NMB kwa niaba ya shule nyingine wilayani Nyasa mkoani Ruvuma

 Katikaati kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini Faraja Ngingo akimkabidhi vifaa vya ujenzi Katibu Tawala waaa Wilaya ya Nyasa Salim Ismalil katika hafla ya kutoa vifaa hivyo iliyofanyika katika shule ya msingi Nangombo ambapo NMB imetoa mabati na misumari vyenye thamani ya zaidi ya shilingi miioni 29.7 kwa shule sita wilayani Nyasa.

Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyasa Salim Ismail akiwakabidhi bati walimu wakuu kutoka shule sita wilayani Nyasa ambao wamepewa msaada wa vifaa vya kuezekea kutoka benki ya NMB

Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyasa Salim Ismalil ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya ugawaji vifaa vya kuezekea vilivyotolewa na benki ya NMB kwa shule sita wilayani Nyasa

Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Faraja Ngingo akizungumza kwenye hafla ya ugawaji wa vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na NMB katika shule sita wilayani Nyasa

 Mtaaam kutoka NMB Kanda ya Kusini Agustino Bayona,akito elimu kwa wanafunzi wa shule ya msingi N angombo kuhusiana  ufunguzi wa akaunti za watoto katika Benki ya NMB

Na Albano Midelo,Nyasa

BENKI ya NMB Kanda ya Kusini imetoa msaada wa vifaa vya  ujenzi vyenye thamani ya Zaidi ya shilingi  milioni 29.7 katika shule sita  zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.

Akizungumza kwenye hafla ya ugawaji wa vifaa hivyo iliyofanyika katika shule ya msingi Nangombo mjini Mbambabay, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini Faraja Ngingo amevitaja vifaa vilivyotolewa na Benki hiyo kuwa ni mabati na misumari kwa ajili ya kuezekea.

Amezitaja shule zilizonufaika na msaada huo ni  shule tano za  msingi  ambazo ni shule ya Nangombo iliyopata vifaa vyenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni tano,shule ya Chiwindi vifaa vya milioni 4.6,Lundo vifaa vya milioni 4.5,Chinula vifaa vya milioni 4.28,Ndingine vifaa vya milioni 6.9 na sekondari moja ya Ngumbo ambayo imepewa vifaa vya milioni 4.28.

“Vifaa hivi tunavyokabidhi leo ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya  jamii,sisi kama Benki tunaowajibu  wa kuhakikisha jamii inayotuzunguka inafaidika kutokana na faida tunayoipata’’,alisisitiza Ngingo.

Amesema kwa miaka kadhaa NMB imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kwa kujikita Zaidi kwenye miradi ya elimu kwa kutoa madawati na vifaa vya kuezekea na sekta ya afya vifaa vya magodoro,vitanda na vifaa vingine vya kusaidia matibabu. 

Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyasa Salum Ismail ameishukuru Benki ya NMB kwa msaada wa vifaa hivyo ambapo amesema benki hiyo imekuwa inatoa misaada mbalimbali serikalini katika sekta za elimu na afya.

Amesema Benki hiyo pia imekuwa inatoa mchango mkubwa kwenye majanga ambapo katika Wilaya ya Nyasa,NMB imeshiriki kutoa vifaa vya huruma yakiwemo majeneza  kwa watu tisa waliopoteza Maisha hivi karibuni kwa ajali ya gari katika kata ya Lumeme.

Ametoa rai kwa  walimu wa shule ambazo zimekabidhiwa vifaa hivyo vya kuezekea kuhakikisha vinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ambapo pia amewataka wazazi na walezi kuendelea kusimamia maadili na nidhamu ya Watoto   wao tangu wakiwa nyumbani.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Pasifiki Mhapa amesema NMB imekuwa karibu sana na jamii katika kuhakikisha kuwa changamoto za elimu na afya zinapatiwa ufumbuzi.

Hata hivyo amesema mahitaji ya kielimu katika Halmashauri hiyo bado ni makubwa kutokana na idadi ya Watoto wanaokwenda shule kuongezeka hivyo Halmashauri inahitaji wadau kama NMB kusaidia katika maendeleo yaa elimu.

Akizungumza kwa niaba ya walimu wa wakuu waliopata msaada wa vifaa hivyo,Mwalimu Mkuu shule ya msingi  Chinula Mwl.Emanuel Chilwa ameishukuru NMB kwa msaada huo  ambao unakwenda kupunguza changamoto ya vifaa vya ujenzi katika shule hizo.

NMB ni Benki yenye  matawi Zaidi ya 230 nchini,ikiwa na mashine za kutolea fedha (ATM) Zaidi ya 780 nchi nzima,wakala Zaidi ya 20,000 na wateja Zaidi ya milioni sita.

By Jamhuri