na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Zanzibar

BENKI ya NMB na Kampuni ya Mwani Zanzibar (ZASCO), zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU), ya ushirikiano, lengo kuu likiwa ni kuliongezea thamani zao la kimkakati la Mwani na kupanua wigo wa mchango wake katika kukuza Uchumi wa Buluu visiwani Zanzibar.

Makubaliano hayo yamesainiwa jijini Dar es Salaam Ijumaa, ambako Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Omar Said Shaaban, alishuhudia Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi na Mkurugenzi Mkuu wa Zasco, Dk. Masoud Mohammed Rashid, wakisainihati hiyo.

Mwani ni aina ya mimeainayoota na kukua kwenye majichumvi (bahari) na majibaridi (mito, maziwa na mabwawa), zao ambalo hutumika kutengeneza bidhaa mbalimbali kama vyakula, juisi, shampoo, sabuni, mafuta ya kupaka, jam ya matunda, dawa za meno, viungo vya chakula na mafuta ya nywele.

Akizungumza kabla ya utilianaji saini huo, Waziri Omar, aliishukuru NMB kwa kuunga mkono juhudi za Serkali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) za kuchakata Sera ya Uchumi wa Buluu, na kwamba wanaamini MoU hiyo baina ya NMB na Zasco, inaenda kulipa thamani zao la mwanikulipiku zao la karafuu.

“Rekodi zinaonesha kuwa bei ya mwaniiliYoongezewa thamani ni kubwa kulinganisha na karafuu, hivyo kwa aina hii ya ushirikiano, mwaniinaendakupiku thamani ya karafuukimapato. Kama kwa muda mrefu karafuuimetupa pesa za kigeni, mwani pia inayo fursa hiyo iwapo tutawekeza vizuri hivi.

“Mwani ni zao la kimkakati na tunaishukuru NMB kuungana nasi katika mkakati huu, tunaamini kwamba ushIrikiano huu wa NMB na Zasco, utatusaidia katika maeneo matatu, ambayo ni kuongeza maendeleo yenye tija kwa wajasiriamali wadogo wadogo wa mwani, kupata mitaji, mikopo na ujuzi ama elimu.

“Kwa sababu ingawawanaosaini makubaliano haya ni ya NMB na Zasco, lakini wanufaika wakuu na wa awali sio wao. NMB na Zasco jukumu lao ni kusapoti kwanza wajasiriamali wadogo ambao ndio walengwa, ndio maana tunaliona jambo zuri linalopaswakuungwa mkono na wadau wengine wa maendeleo

“Tunaishukuru NMB kwa ‘engagement’ nyingi mnazofanya, na miminiwahakikishie kwamba SMZ kupitia wizara yangu, tunaona na kuthamini jitihada zenu zote katika maeneo mbalimbali zinazochochea Uchumi wa Zanzibar na kuisaidia serikali kutekeleza mikakati yake,” alisisitiza Waziri huyo.

Waziri wa Biashara na maendeleo ya Viwanda Zanzibar,  Omar Said Shaaban (katikati) akishuhudia kubadilishana kwa makubaliano ya ushirikiano kati ya Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wapili kulia) kwa niaba ya Benki na Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Mwani Zanzibar (ZASCO), Dkt. Masoud Rashid Mohamed katika makao makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es salaam Kulia ni meneja wa biashara za Zanzibar wa Benki ya NMB, Naima Shaame na kushoto ni Mkuu wa idara ya Kilimo wa Benki hiyo, Nsolo Mlozi.

Awali, Mponzi aliipongeza SMZ chini ya Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi, ambaye maono yake ya kukuza Uchumi wa Bluu, yaliivutia NMB na kuwasukuma kufanya makubaliano mbalimbali ya ushirikiano, siri ya hilo ikiwa ni mazingira wezeshiyanayojengwa na serikali yake.

“Serikali ya Awamu ya Nane, NMB tuko katika kasi kubwa kusapoti jitihada hizo, ndio maana mwaka jana tumefungua matawi na vituo kadhaa, mwaka huu pia tutaongeza matawi matatu Zanzibar ya Nungwi, Wete, na MjiMkongwe ili kutanuawigo wa kuwahudumia wazanzibar.

“Katika zao la mwani, tangu awamu hii ilipoonesha dira yake na tukavutiwa nayo, tukaanza kutoa elimu za fedha kwa wakulima wa mwani, wakulima wa chumvi, wavuvi na wajasiriamali wengine, ambakowaliokidhivigezowalikopesheka fedha na vitendea kazi.

“Kwa hiyo leo wizara yako inapokuja na Zasco kwa lengo la kuongeza thamani ya zao hilo na ajira kwa ujumla, tukaona ni mkakati mzuri na kuamua kujitoa kuingia makubaliano haya kuwawezesha wakulima na kukuza Uchumi wao na taifa kwa ujumla,” alisisitiza Mponzi.

Aliongeza ya kwamba, MoU hiyo inaenda kuwawezesha wakulima wa mwaniwafanye kazi kwa ufanisi, kupata mazao kwa wingi na waweze kunufaika pundewatakapoyapelekaZascokuongezewa thamani, jukumu lao kubwa likiwa ni kuwanoa wakulima bure na kuwapa elimu ya masuala ya fedha na biashara.

“Jinginetutahakikisha kwamba tunawafikia wakulima wa mwani kote waliko, hata vijijini huko, tutawafikiatukiwa na masuluhisho yote ya kifedha, ambapo pia tutawafikishia huduma zetu zote zikiwamo wakala na huduma mpya sokoni hivi sasa ya NMB Pesa

“Hii ni akaunitiinayokwendakushughulikapakubwa na wakulima, wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo, ambao watapata manufaa kupitia akaunti hii isiyo na makato ya kila mwezi, ikiwamo mikopo ya Mshiko Fasta ya kuanzia shilingi 1,000 hadi 500,000 bila fomu, wala viambatanishi vya dhamana,” alisema.

Alitoa kwa Wazanzibar kuchangamkia huduma jumuishi za kifedha kupitia NMB Pesa, wafungue akaunti ili kuendelea kuunga mkono juhudi za benki hiyo ilizoonesha katika MoU mbalimbali walizosaini kwa nyakati tofauti.

Mponzi akaongeza kwamba: “Makubaliano hayo ni mkakati wa NMB katika sio tu kuboresha huduma zake, bali pia kuongeza mchango wa sekta ya kilimo, huku ikisaidia kukuza Uchumi hususani kwa hapa Zanzibar, mahali ambapo NMB tunajivunia kuwa sehemu ya ukuaji wa Uchumi wa Buluu.”

Naye Mkurugenzi wa Zasco, alisema anaishukuru NMB kuona umuhimu na haja ya kuungana na kampuni yake iliyoanzishwa kimkakati na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda katika kunyanyua zao la mwani, kwani makubaliano haya yanaendakukipa thamani kilimo hicho.

“Tunawashukuru NMB huku tukiahidi utekelezaji wa makubaliano yote yaliyomo ndani yake, tukiamini kwamba mashirikiano haya yamebeba dhima kuu ya uendelezaji wa wakulima na zao la mwani kwa ujumla. Baada ya MoU hii, sasa ni utekelezaji tu.

“Zascoimeanzishwa na SMZ chini ya Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda, ni kampuni changailiyopewa majukumu makubwa na muhimu katika ustawi na uwekezaji wa kuongeza thamani ya zao la mwani.

“Kwa zaidi ya miaka 30 Zanzibar kampuni zilinunuamwanimkavu na kusafirisha nje ukiwaghafi, hivyo kufanya malipo anayolipwamkulima kuwa ni madogokulinganisha na uwekezaji aliofanya, ndipo SMZ ikaonamwarobaini wa hili ni huanzishwaji wa Zasco ili kuongeza thamani na kunyanyuapato la wakulima

Kampuni hii licha ya uchanga lakini imefanikiwa kuanzisha kiwanda cha kuchakata bidhaa iitwayo ‘carrageenaan’, kiwanda hiki kitakuwa kikubwa zaidi Afrika chenye uwezo wa kuchakatamwani yote inayozalishwazanzibar,

“Makubaliano haya yamekuja wakati muafaka kabisa, kwa sababu Zascoimejengakiwanda kikubwa zaidi Afrika, ambacho uwezo wake ni mkubwa sana kuchakatatani 30,000, lakini uzalishaji wa mwani Tanzania ni mdogo sana tani 12,000, nguvu za ziada zinahitajika, ili kuongeza uzalishaji ndio maana tunafurahishwa na ushirikiano huu na NMB,” alisema.