Nyerere: Tunamtaka rais anayechukia rushwa

“Rushwa ni adui wa haki. Tunamtaka rais atakayelitambua hilo, atakayeichukia rushwa hata ukimwangalia aoneshe kweli anaichukia rushwa, sio rais anayesema kweli rushwa ni adui wa haki… lakini ukimwangalia usoni unashangaa na kusema… aaaah kweli huyu?”

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Margaret Chan: Mafua ni hatari duniani

“Magonjwa ya mafua lazima yaangaliwe kwa umakini, kwa sababu ya uwezo wake wa kuenea kwa kasi katika kila nchi duniani.”

Haya yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya duniani (WHO), Margaret Chan.

 

Bernard Membe:

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inathamini uhusiano uliopo baina ya Tanzania na Malawi, na ina dhamira ya kudumisha na kuimarisha ujirani mwema kwa manufaa ya watu wetu.”

Haya yalinenwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

 

Tibaijuka: Tusimrundikie mwananchi mzigo wa nyumba

“Kumrundikia mtu malipo na kumtegemea ajenge nyumba mwenyewe kuna upungufu kwani inamaanisha atafute eneo jipya na ajenge. Mchakato huu hupoteza muda na kusababisha fidia yake kupungua thamani.”

Hii ni kauli ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Tanzania, Profesa Anna Tibaijuka.

Please follow and like us:
Pin Share