Julius Nyerere: Mahitaji ya wananchi yalindwe

“Lazima tuendelee kuhakikisha kwamba mahitaji ya msingi ya watu wote yanapatikana na yanalindwa. Lengo letu lazima liendelee kuwa kuinua hali ya maisha ya kila mtu, na kila mtu aweze kupata huduma za msingi za elimu na matibabu.”

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Michelle Obama: Wahudumie watu kwa hadhi

“Wahudumie watu kwa hadhi na heshima, hata kama hauwafahamu, na hata kama haukubaliani nao.”

Haya ni maneno ya Michelle Obama, Mke wa Rais Barack Obama wa Marekani.

 

Nelson Mandela: Elimu ni silaha kubwa

“Elimu ni silaha yenye nguvu kubwa ambayo unaweza kuitumia kubadilisha Dunia.”

Haya yalisemwa na Rais wa kwanza Mwafirika wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.

 

Joyce Banda: Wanawake wa Kiafrika tunaweza

“Ni mzigo mzito [urais], lakini ninaweza kuubeba. Kwanini? Kwa sababu mimi ni mwanamke wa Kiafrika. Wanawake wa Kiafrika hubeba mizigo mikubwa.”

Kauli hii ni ya Rais wa Malawi, Joyce Hilda Banda. Ni rais wa taifa hilo tangu Aprili 2012.

Please follow and like us:
Pin Share